Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Japokuwa uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupindukia ni moja ya tabia zinazosababisha hatari ya aina kadhaa za saratani ikiwemo saratani ya mdomo, kwa miaka ya karibuni, idadi ya wagonjwa wa aina mbalimbali za saratani imekua ikiongezeka kwa kasi ikihusishwa na maambukizi ya aina fulani ya virusi vinavyosababisha aina nyingi za saratani. Aina hii ya virusi kitaalamu inajulikana kama Human Papillomma Virus (HPV).
 
HPV ni moja ya virusi vinavyopatikana kupitia ngono ya aina yoyote. Japo takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi haya siyo makubwa Tanzania, tunashauriwa kuchukua tahadhari na hasa kutokana na taarifa zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), hivi karibuni ambazo zinaonya kuwa watu wa Afrika Mashariki wako hatarini kupata maambukizi ya HPV na hii yote ikisababishwa na vitendo vya ngono visivyo salama na hasa kwa kuhusisha midomo.
 
Virusi vya HPV mara nyingi havionyeshi dalili yoyote. Mtu aliyeambukizwa na virusi anaweza asijue kama ameambukizwa hata kwa miaka kadhaa kabla havijasababisha saratani.

Uhusiano hasa upo hivi, virusi hivi hutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia ngono ambayo kwa namna yoyote kama ikitokea kugusana kati ya ngozi na ngozi na hasa mdomo na via vya uzazi. Lakini naomba ifahamike pia hata kufanya ngono kwa njia ya kawaida pasipo kuhusisha midomo bado inaweza kusababisha hatari ya maambukizi ya virusi hivi na dhana ni ileile kama ilivyo kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi na hasa isiyo salama.
 
Hili linawahusu pia hata wanaofanya ngono kinyume na maumbile. Kupitia kufanya ngono kunakohusisha mdomo, kunasababisha maambukizi ya virusi hivi kwa kuwa ni rahisi zaidi na husababisha kwa kiasi kikubwa saratani za mdomo na za koo.

Japo wakati mwingine hutokea virusi hivi hufa vyenyewe, lakini kwa watu wengine baada ya maambukizi, hukaa na kutengeneza makazi ya kudumu kwa miaka kutokana na mfumo wa kinga za mwili kuwa hafifu na hukaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili ambazo wakati wote zinakuwa laini na hasa ukeni, mdomoni na kooni.
 
Back
Top Bottom