Hili linawahusu pia hata wanaofanya ngono kinyume na maumbile. Kupitia kufanya ngono kunakohusisha mdomo, kunasababisha maambukizi ya virusi hivi kwa kuwa ni rahisi zaidi na husababisha kwa kiasi kikubwa saratani za mdomo na za koo.
Japo wakati mwingine hutokea virusi hivi hufa vyenyewe, lakini kwa watu wengine baada ya maambukizi, hukaa na kutengeneza makazi ya kudumu kwa miaka kutokana na mfumo wa kinga za mwili kuwa hafifu na hukaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili ambazo wakati wote zinakuwa laini na hasa ukeni, mdomoni na kooni.