Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inaweza kuchukua miaka zaidi ya hata 10 tangu maambukizi haya kugeuka kuwa saratani mwilini, hivyo unaweza ukafanya ngono kwa kupitia mdomo leo na kupata maambukizi ya virusi na vikakaa mwilini na hatimaye vikishafanya makazi ya kudumu ndipo vinageuka na kuwa saratani miaka kadhaa ijayo.

Watu wengi waliugua saratani zinazotokana na maambukizi ya virusi hivi miaka kadhaa iliyopita. Hivyo ninawasihi vijana ambao ndio waumini wakubwa wa tabia hii ya kunyonya via vya uzazi wakati wa tendo la ndoa, wanaweza wakafurahia, lakini vikaja kuwaletea madhara makubwa miaka kadhaa ijayo.
 
Kama nilivyosema hapo awali, HPV vinasababisha saratani za aina nyingi, lakini kupitia ngono inayohusisha midomo hasa inasababisha saratani za mdomo na koo na ni vyema kuzifuatilia kwa ukaribu dalili za saratani hizi kama vile majeraha madogo ya mdomo ya mara kwa mara kwa mara, michubuko yenye rangi nyeupe ya sehemu ya ndani ya mdomo na kooni, uvimbe unaoota mdomoni au kooni, maumivu ya mara kwa mara ya mdomoni, ndani ya shingo na kooni, kupata shida ya kumeza na kuhisi maumivu wakati wa kumeza kitu au maumivu kwenye taya pamoja na maumivu na muwasho kooni ya mara kwa mara.
 
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa na malalamiko ya kila aina ya wanandoa kutokuwa waaminifu. Wapo waliokabiliana na misuguano, mapigano na ugomvi mwingi kwa sababu ya jambo hili na wapo ambao tayari wameshaamua kutengana.

Watoto wa familia nyingi wamebaki kuwa waathirika wa tatizo hili na bado hakuna dalili za tatizo hili kupungua.

Kila mmoja akiulizwa anatoa sababu yake binafsi ya kwa nini ametoka au alitoka nje ya ndoa. Sababu hizi zina mfanano na baadhi zinatofautiana.
 
Katika makala hii nimejaribu kuangalia baadhi ya sababu ambazo mara kwa mara zimeripotiwa na wanandoa wengi wanaokuja kwenye ushauri kwenye ofisi zetu. Hii inafanya sababu hizi kuwa halisi na zitakazokupa msaada ukizielewa maana haziko kinadharia tu, bali zimetokea katika maisha halisi ya ndoa za watu kama wewe.

Pamoja na yote haya ukweli unabaki kwamba matendo ya kukosa uaminifu kwenye ndoa au mahusiano yana athari mbaya sana na athari hizi zinaweza kuambatana na maumivu makali na wahusika kuwa maadui badala ya wapenzi kama walivyokuwa awali.
 
Kutoridhishwa katika tendo la ndoa

Kumekuwepo na malalamiko mengi na tofauti baina ya wanandoa wanaume na wanawake katika suala hili.

Wanaume wanalalamika kwamba wake zao mara baada ya kuolewa na hususan wakishapata watoto wanaanza kuwa wazembe na wasiojituma kwenye tendo la ndoa kama walivyokuwa awali.

Tafiti zinaonyesha kwamba mara mwanaume anapohisi kutoridhishwa kwenye tendo la ndoa ana nafasi kubwa zaidi ya kutoka nje mapema kuliko mke wake. Wanawake wana uvumilivu wa ziada na kwa wale waliotoka nje ya ndoa zao walifanya hivyo baada ya uvumilivu wa miaka mingi na kukosa tumaini.
 
Kutoridhishwa katika tendo la ndoa kunaweza pia kusababishwa na maumbile ya mwili, kwa mfano watu wenye miili mikubwa na uzito mkubwa hupata shida kuwaridhisha wenza wao ukizingatia kwamba tendo la ndoa ni zoezi la kimwili.

Mtu wa jinsi hii anaweza kushindwa kwa sababu ya ukubwa wa mwili, kuutuma mwili wake kadri anavyotaka na pia wengine kuishiwa pumzi au kuchoka mapema na hivyo kufika kileleni mapema.

Hali hii husababisha kutoridhika kwa wanawake wengi kwenye ndoa. Sababu nyinginezo zilizotajwa za wanandoa kutoridhishana kwenye tendo la ndoa ni kama vile uchafu, harufu zisizo nzuri, uelewa mdogo wa namna ya ufanywaji wa tendo, makuzi na mapokeo, mambo yanayohusiana na mila, utamaduni au imani pamoja na magonjwa.
 
Kutokupata tendo la ndoa kwa muda mrefu

Waathirika wa sababu hii ni wanaume kuliko wanawake. Tunaposema muda mrefu, hili ni suala tofauti kwa mwanaume na mwanamke. Kwa mwanaume wiki moja yaweza kuhesabika ni muda mrefu kulingana na mazoea yaliyokuwepo kwenye ndoa hiyo.

Kisayansi na kibaiolojia, mwanamke ana uwezo wa kustahimili au kuvumilia kukaa bila kufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu kuliko mwanaume.

Baadhi ya tafiti pia zimeonyesha kuwa watoto wengi wa nje ya ndoa wanazaliwa katika vipindi ambavyo tendo la ndoa lina shida, hii inamaanisha nyakati za ugonjwa, ujauzito, ugomvi au vipindi vingine vilivyofanya mwanaume asipate tendo la ndoa ndipo ambapo aliamua kwenda pembeni na huko kukatokea mimba na baadaye mtoto.
 
Utaelewa ukubwa au kiasi cha tatizo kwa kuangalia ukweli kwamba kwenye ndoa nyingi, wanaume ndio wanaoongoza kwa kuwa na watoto nje ya ndoa na si wanawake.

Katika jambo hili la kutokupeana tendo la ndoa kwa muda mrefu, tumekuwa tukishauri kwamba kila mwanandoa ahakikishe anaweza kuzuia migogoro isiathiri tendo la ndoa ili wasikae muda bila kulifanya, na kama kuna safari au utengano wa lazima baina yao basi kuwepo na mawasiliano ya mara kwa mara na ikibidi wanandoa watembeleane au kuwa pamoja zaidi ya kutokuwa pamoja.

Umbali una athari kubwa sana kwenye ndoa nyingi. Kwa mara nyingine niseme hili, kunyimana tendo la ndoa kama adhabu au kwa matakwa yoyote binafsi hakujengi bali kunabomoa kwa sababu wengi wamejikuta wakitoka nje ya ndoa zao kwa sababu hii.
 
Jaribu kufanya utafiti hata sasa hivi. Zungumza na mwanamke yeyote yule, mama yako, mkeo, mwanao, dada hata shangazi awe mwanamke tu.

Kisha muulize swali lolote lililo karibu yako ambalo litamuhusu yeye.

Labda muulize anapenda kufanya nini siku za mapumziko? Au anapenda kuvaa nini? Muulize chochote tu, halafu sikiliza jibu atakalokupa, kisha tumia uzoefu wako wa namna unavyomfahamu kuona kama linafanana naye.
 
Majibu ya wanawake karibu wote duniani ni kama sarafu, yana pande mbili, bichwa na mwenge.

Kama unataka kujua kitu kuhusu mwanamke, na ukatumia majibu yake vile vile yalivyo basi jua unajiuza mwenyewe, hutopata anachomaanisha au unachostahili kukielewa.

Wengi ukitazama upande wa pili wa jibu lao, utagundua kuwa aidha anachokijibu sio ambacho anafikiria, au pengine jawabu alilokupa limekuja tu kwa sababu hana anachofahamu juu ya swali ulilomuliza— japokuwa linamuhusu mwenyewe.
 
Mfano baadhi ya wanawake wakiulizwa wanapenda kuolewa na mwanaume gani, anaweza akakupa majibu ya ajabu hadi mwenyewe ukashangaa.

Anaweza kukwambia anapenda mwanaume mrefu, asiwe anavuta sigara, asiwe anakunywa pombe, ajue kupika, awe msomi kidogo, awe na upendo, awe anajua kuvaa, awe anatabasamu, awe anapenda watoto, awe hachelewi kurudi kazini, awe anampenda Mungu, asiwe mnene, awe anafanya maozezi na zaidi na zaidi na zaidi.
 
Na hapo usikute pengine upande wa pili anachopenda zaidi ni mwanaume mwenye pochi nzuri tu, au labda hajui hata anachokipenda kwa hiyo anajikuta ana msururu wa majibu.

Tabia ya majibu ya mwanamke kuwa kama sarafu ndiyo inayosababisha ukitoka na mwanamke yeyote atumie saa nane kuvaa kwa sababu hajui nini cha kuvaa.

Unakuta kabati limejaa nguo lakini zote anaona kama hazimtoshi, sio kwa sababu anapenda fasheni, ni kwa sababu wakati ananunua hakuwa akifahamu nini anapenda, sasa hata wakati wa kuvaa anakuwa na wakati mgumu kujua nini anataka.
 
Ndiyo maana wataalamu wanasema, mwanamke akikujibu Hapana, basi kaa ukijua hapo kuna ndiyo kubwa nyuma. Majibu ya wanawake hayana upande mmoja.

Hata mkitoka, ikafika kwenye hatua ya kuagiza chakula, unaweza ukaagiza unachotaka na yeye akaagiza chake, lakini vikishashushwa mezani, akataka kujaribu na chako.

Sio kwa sababu ni mroho, hapana ni vile tu wakati anachagua cha kula hakuwa akifahamu anataka kula nini.

Tabia ya kutokujua hata wanaume tunayo, lakini kwetu ni afadhali. Ndio maana mwanaume akiulizwa swali ambalo labda hana jibu anakuwa muwazi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…