Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
*ASILI HAIFI*
 
Ni ajabu kwamba makubaliano ya kumtoa mtoto mlemavu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi ya kuombaomba mjini iliafikiwa na wazazi na kubarikiwa na kiongozi wa kijiji.

Maelezo ya Mama Pili kuwa kiongozi wa kitongoji alisaini makubaliano ya kumchukua mtoto huyo mlemavu wa kichwa kwa ajili ya kwenda kuomba jijini Dar es Salaam, yananifanya nimtafute kuthibitisha habari hizo.

Siku iliyofuata nilimtafuta kiongozi niliyeambiwa alisaini makubaliano ya tajiri huyo na Baba Pili. Kiongozi huyo wa kitongoji, ambaye anaitwa William Nullu, alikubali kuwa ndiye aliyesaini makubaliano hayo ili kuisaidia familia hiyo.
 
Siku moja asubuhi nikiwa nyumbani, alikuja kijana wa Iyobhe na kuniambia baba yake ananiita,” anasimulia.

“Niliitikia wito na kuelezwa kuna mtu anaitwa Nyanda anataka kumchukua Pili aende naye Dar es Salaam kufanya kazi ya kuomba.”

Anasema kutokana na maelezo ya wazazi wote wawili na yule kijana Nyanda, aliamua kuruhusu mtoto huyo achukuliwe, lakini hakujua kama anachoenda kufanyiwa mtoto huyo ni kosa.
 
Ujue dada sisi wenyeviti wa vitongoji na vijiji tulioko huku vijijini hatuna elimu ya kutosha,” ananiambia.

“Hakuna tulijualo. Mimi alipokuja huyo mtu niliona ni jambo zuri na kuidhinisha aondoke. Niliona nitaisaidia hiyo familia ambayo inaonekana kwenye umaskini.”

Anasema kuchukuliwa Pili ni sehemu ya wimbi kubwa la watu kutoka mjini kufika kijijini hapo kuomba walemavu na kuondoka nao. “Wapo wengi tu, hata juzi kuna mmoja alikuja alikuwa anamtaka mlemavu mmoja yuko Ngapo pale. Sasa sijui walishindwa kuelewana na mzazi? Naona bado yupo na hawajaja kwangu,” anasema.
 
Mwenyekiti wa kitongoji hiki anadai kuwa kinachosababisha wazazi kuruhusu watoto wao walemavu ni umaskini. Alisema pia mashindano ya kumiliki ngombe wengi, huchangia suala hilo.

“Ukiwa na ng’ombe huku kwetu unaheshimika. Hata Mzee Iyobhe nilipokaa naye siku moja, aliniambia anataka pesa itakayokuwa inatumwa kwa kazi ya Pili anunue ng’ombe ambazo zitamsaidia Pili kuishi maisha mazuri hata kama ikitokea Iyobhe amekufa,” anakumbuka.

Mwenyekiti huyo anasema Iyobhe anaamini mtoto mlemavu huishi maisha magumu wazazi wake wanapofariki, anaweza kutengwa na ndugu. “Hivyo ukiwa na ng’ombe wengi ndugu watakuja kwake na watamsaidia kwa sababau ana mali,” anasema.
 
Ofisa maendeleo wa wilaya ana taarifa

Maelezo ya kiongozi huyo wa kitongoji, yananifanya nitafute ufafanuzi kutoka kwa ofisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Shinyanga Vijijini, Joramu Enock, ambaye anasema aliwahi kupata taarifa za kuwepo kwa biashara hiyo.

“Sikuchukulia (taarifa hizo) kwa uzito, lakini naomba nilifanyie kazi,” anasema na kuahidi kuwasiliana na Jeshi la Polisi.

Mradi huo pia una watu wanaoufanikisha kwenye kijiji hicho
 
Nikiwa jijini Dar es Salaam nilionana na mmoja wa watu wanaofanya biashara hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Gazi, mwenyeji wa Kijiji cha Nindo wilayani Shinyanga Vijijini.

Gazi, ambaye pia anajishughulisha na uganga wa kienyeji akidai kuwa huwezesha watu kuwa matajiri kishirikina, ndiye mganga anayeaminiwa na watu wengi wanaofanya biashara hiyo.

Gazi pia anadai ana mlemavu mmoja na anatarajia kwenda kijijini kwao kuongeza walemavu wengine wawili ili kuongeza nguvu ya pesa.
 
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nataka Ramadhani inikute nimejipanga, ujue kujipanga,” anasema akidai mwezi huo ndio huwa wanavuna pesa nyingi ikilinganisha na siku nyingine.

Mfanyabiashara huyu ambaye pia nilifanya jitihada za ziada kumpata, anasema ni miaka miwili sasa tangu aingie kwenye mradi huo.

Lakini anasema yeye ni mganga hodari anayewasaidia watu wanaomiliki walemavu kufanikisha biashara hiyo ya kuombaomba.

Anasema pia ndiye anayewatibu kwa dawa za kienyeji wakati walemavu hao wanapougua.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] JASIRI HAACHI ASILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…