Fikiri na mimi, mfano mtu najua kuwa kuvuta sigara ni hatari kwa afya yake ni hatari lakini bado anavuta, ukiongea nae atakwambia najitahidi kuacha lakini siwezi.
Au mtu anajua kufanya ngono ni hatari kwa maisha yake lakini anashindwa kuizuia tamaa yake na kujikuta katika matatizo makubwa.
Tambua kuwa mwenye dhamana ya maisha yako ni wewe mwenyewe, na ukijiamini na kusimamia haki hata jamii yako nayo unayoihofu siku zote itkuheshimu pasipo wewe kutumia nguvu nyingi kuwaonyesha kuwa unastahili kuheshimika.
Uwezo huu wa kuamua kuwa mshindi upo ndani yako, na ukiamua kuutumia vema utakuwa mshindi kila leo na katika nyanja zote uzijuazo. Lakini ni hadi uamue kuwa na msimamo kwako mwenyewe, yaani sio kuwa na uwezo wa kuwazuia wengine wasifanye huku wewe uwezo huo hauna wa kujizuia.