2.Deni la mazingira
Mungu alimtwaa Adamu akamweka katika Bustani ya Eden Ailime na kuitunza . Adamu wa leo ni wewe na Mimi je, unafahamu kuwa umefungwa ufahamu wako kwa kutokufanya usafi wa mazingira na Akili yako imelala haiwezi kufikiri mambo makubwa bali inafikiria vitu vya kawaida kila siku ? Kugusa ardhi ni kufungulia baraka , ulinzi wa kazi zako, kuanza kuona fursa mbalimba. Ni kuanza kuwa na furaha, Amani ndani yako, inakusaidia wewe na mimi tutumie muda vizuri. Badala ya kuongea umbea , kuangalia movies siku nzima, kuchart na kusoma magazeti , tumia muda wako kufanya usafi wa mazingira, nyumbani mwako, kazini kwako, barabarani, kuzibua mitaro na vingine vingi, utaanza kuona Mungu anakushirikisha baraka zake.