Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kujijali ni kitu gani? ni hali ambayo inahitaji kupata muda wa kutulia ukiwa mwenyewe kwa ajili yako na maendeleo ya maisha yako badala ya kusubiri mtu mwingine kukujali wewe.
 
Mara nyingi watu wanauliza unawezaje kujijali ukiwa na majukumu ya kuhudumia wengine ? Jibu ni kwamba , huo ni mtazamo wa mtu . Lakini kama utafahamu kutumia muda wako vizuri unaweza kuchukua nafasi kwa ajili yako. Unatafuta muda katikati ya muda wako kutulia kila siku kwa dakika kadhaa mahali ambapo pana utulivu ili kuongeza nguvu mpya, mawazo mapya . Utatumia muda wako kwa kukaa tu bila ya kufanya kitu , ukiwa umetulia .
 
2.Kujijali maana yake ni jinsi unavyojiona mwenyewe.

Kujua matumizi ya muda, kufafamu muda wako wa kupumzika na wa kulala na muda wako wa kufanya kazi , Kufahamu ratiba yako ya kila siku, ya wiki, ya mwaka. Na kufahamu jinsi ya kutunza mwili wako , Akili yako na Roho yako. kujipenda, kujithamini, kujiona mshindi kuanzia ndani mwako.
 
3.Kujijali ni Kumpenda Mungu, Kuwapenda watu na kuipenda nafsi yako.

Chochote unachopenda ufanyiwe wewe, jaribu kuwafanyia wengine. Ukimpenda Mungu kwa nguvu zako zote, akili yako yote, moyo wako wote na roho yako yote, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Kuacha kula vitu ambavyo sio salama kwa afya yako. kuacha dhambi ili kuondokana na hofu , mashaka mbalimbali kwenye maisha yako.
 
4.Kujijali maana yake ni Kuishi Wakati Uliopo

Watu ambao wanasubiri kufanya kitu baadae , hawajijali na wala hawajitambui. Una masaa 24 kila siku kwa nini usitumie muda wako kufikiri mambo yaliopo wakati huo. Utakuta mtu ana kitu cha kufanya lakini anasema nitafanya kesho, wakati uwezo wa kufanya hicho kitu anao. Unapoteza muda mwingi sana . Utashindwa kujijali mwenyewe. Kama huna Nidhamu ya mitandao huwezi kuishi wakati uliopo. kama hutumikishi mwili wako sawasawa hutaweza kuishi wakati uliopo. Watu wengi wanaugua magonjwa ya kutofanya kazi za kutosha.
 
Back
Top Bottom