Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mungu hampi mtu pesa asiyekuwa na maarifa na ufahamu. Asiyekuwa na Hekima. Mungu anakupa pesa kulingana na akili , na uwezo ulionao wa kufikiri. Utalalamika sana, utaomba sana, utafunga sana, lakini kumbuka kuwa ,
 
Kuna madeni makubwa ambayo wana wa Nuru hawayafahamu , Nayo ni madeni ya kiroho. vifurushi vikubwa.

1.Deni la Muda

Mungu anakupa masaa 24 kila siku lakini haupo tayari kujifunza maarifa ya nenbo la Mungu. hauko tayari kwenda kuwatazama Yatima, Wajane, Wafungwa, Husomi neno la Mungu, Huandiki neno la Mungu. Muda wako mwingi unapotelea kwa adui. upo tayari kukaa bar masaa matatu na zaidi , kijiweni, kwenye smartphone kuchart na kusambaza dhambi zilizojificha, halafu unajiita mwana wa Mungu. Hutaweza kufanikiwa. Wakati huo huo wana wa giza wako bize kupigana na maisha wewe umelala.
 
2.Deni la mazingira

Mungu alimtwaa Adamu akamweka katika Bustani ya Eden Ailime na kuitunza . Adamu wa leo ni wewe na Mimi je, unafahamu kuwa umefungwa ufahamu wako kwa kutokufanya usafi wa mazingira na Akili yako imelala haiwezi kufikiri mambo makubwa bali inafikiria vitu vya kawaida kila siku ? Kugusa ardhi ni kufungulia baraka , ulinzi wa kazi zako, kuanza kuona fursa mbalimba. Ni kuanza kuwa na furaha, Amani ndani yako, inakusaidia wewe na mimi tutumie muda vizuri. Badala ya kuongea umbea , kuangalia movies siku nzima, kuchart na kusoma magazeti , tumia muda wako kufanya usafi wa mazingira, nyumbani mwako, kazini kwako, barabarani, kuzibua mitaro na vingine vingi, utaanza kuona Mungu anakushirikisha baraka zake.
 
3.Deni la UPENDO

Kumpenda mke, mume, kuwapenda watoto, kuwapenda majirani, kujitoa kwa ajili ya wengine. kumpenda Mungu, Kujipenda wewe mwenyewe.
 
4.Deni la Kutoa

Kutoa ni lazima kwa sababu tunatakiwa kuonyesha upendo kwa Mungu. Mungu alitupenda na akawa mfano kwetu katika kutoa. Tusipotoa tunaharibu Agizo la Mungu , Tunaruka maandiko ya Mungu. Mungu hawezi kukushirikisha Baraka zake Kama humtolei kwa moyo wa kupenda. Mungu hawezi kuweka ulinzi kwenye mali zako, hawezi kuweka ulinzi wa kazi zako na familia yako pamoja na vitu mbalimbali katika maisha yako.
 
Lakini wana wa giza wanatoa sana kwa Mungu wao , Ndio maana wanafanikiwa. Hata kama kitu ambacho kinamuumiza moyo anakitoa .Mfano kuua mzazi, watoto, mke na ndugu.
 
Kaa fikiria kama Mungu angesema kila mtu awe ananunua pumzi, ingekuwaje? maana kila siku inawezekana tungekuwa tunaenda kujipanga makanisani au misikitini ili kununua Pumzi. Sidhani kama watu wangeweza kupona , maana watu wengi hawana uwezo wa kununua .
 
Huwezi kumpenda Mungu kama hutoi muda wako kumtumikia , hutoi pesa kusaidia wengine, unajiangalia wewe.

Badilika , anza kutumia muda wako vizuri, anza kumpenda Mungu, Fanya usafi wa Mazingira. Wapende watu na kuipenda nafsi yako. ukiwapenda watu hutawafanyia vibaya, hutawaua kwa kuwauzia vitu hatari ambavyo wewe mwewnyewe huwezi kuvitumia. hutaweza kuwawazia mabaya.
 
uenda unahisi hakuna kitu kizuri mbele yako. Unatamani muda uishe haraka uende kulala tena . Huenda unahisi kitu kilichotokea kwako kama ndoto ya mchana. Ni kwa sababu huna kitu cha kufanya.
 
Ni mtazamo wako unatesa akili yako . jinsi unavyojisikia unavuta hali ile ile ya watu wakuone jinsi ulivyo. Unajihisi kama hakuna kitu kinachowezekana kwako zaidi ya kurudi kulala au kwenda kulewa. Lakini sio kweli. Mara zote kuna kitu cha kufanya.Ni kwa sababu bado uko gizani, Toka gizani nenda kwenye Nuru.
 
Acha kulalamika kwa sababu zipo kazi mamilioni ambazo unaweza kufanya bila hata ya kumuomba mtu kwa kutumia muda wako tu. Kila siku anza na ratiba yako, unaweza kujifunza kitu ambacho hujawahi kufanya. unaweza kusoma vitabu, unaweza kwenda kwenye semina mbalimbali. Unaweza kwenda baharini kama mahali ulipo kuna bahari. unaweza kutoka na kutembea kwenye Nature. Unaweza kujifunza kupika chakula ambacho hujawahi kupika. Unaweza kuanza mazoezi .Fanya kitu chochote ambacho utakiweza.
 
Hata kama hujisikii kuvaa hata nguo, hata kama hujisikii hata kusogea, unao uwezo wa kujilazimisha kufanya hivyo. Ondoka kwenye hali hio. Usipoteze siku yako, tengeneza siku yako. Kwa sababu utakapopoteza siku moja ndivyo ambavyo utapoteza siku inayofuata. Usipende kukaa mahali salama kila wakati, unapoteza muda wako. Usipende maisha ya kawaida wakati una uwezo wa kuishi maisha ya juu.
 
Maisha yako yasiwe na mazoea ya kuamka na kwenda kazini au shuleni na kurudi tena kulala. Pata muda wa kukaa na kufikiri kujiboresha zaidi ya unachokifanya kwa siku nzima. Hisi kama unatembea huku umelala wiki nzima.

Fanya kitu leo, pata kitu ndani ya siku yako, ili ujisikie kuwa mtu bora Duniani, kwamba una faida ya kuwepo hapa. Kwa sababu utatambua kuwa hukutumia muda wako vibaya.
 
Maisha yako yasiwe na mazoea ya kuamka na kwenda kazini au shuleni na kurudi tena kulala. Pata muda wa kukaa na kufikiri kujiboresha zaidi ya unachokifanya kwa siku nzima. Hisi kama unatembea huku umelala wiki nzima.

Fanya kitu leo, pata kitu ndani ya siku yako, ili ujisikie kuwa mtu bora Duniani, kwamba una faida ya kuwepo hapa. Kwa sababu utatambua kuwa hukutumia muda wako vibaya.
 
Fanya mazoezi kwa dakika 40 na kuendelea, jibu simu ambazo umekuwa ukizikataa, jibu meseji, Fanya Usafi, Fanya kitu cha upendo kwa mtu mwingine, utaona furaha inakaa kwako. Jipongeze mwenyewe.
 
Usisubiri Kesho kukamilisha lengo lako. Vitu vikubwa huchukua muda kukamilika, havitokei kwa usiku mmoja. Itakuchukua miaka kadhaa kufika lengo lako. Kama kila kazi zako unaziweka ili ufanye wiki ijayo au mwaka ujao, hutakaa ukamilishe lengo lako.
 
Huwa ni ngumu sana kusubiri kitu, lakini ni rahisi kukaa muda mrefu bila kufanya kitu, Lakini kumbuka kukaa bila ya kufanya kazi sio afya. Jitoe muhanga kama unataka kufanikiwa maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…