Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hint.Hawana muda na nywele au makeup zao. sio zaidi..

Kama wewe ni moja wa wanawake wa kisasa, nafikiri unajisikia sawa kabisa kumwalika mwanaume kutoka nae kwa siku za leo.
 
Inawezekana ukawa unahisi kwa njia moja ya sababu hizi.

1.Ulishaambiwa kuwa wanawake na wanaume wote ni sawa, kwa hio huoni sababu yeyote nzuri ya kutofanya hivyo na hasa kama umevutiwa nae.
 
2.Mwanaume uliovutiwa nae, na yeye pia umemvutia, lakini anachukua muda mrefu kukuambia mtoko wote. ulishaona hilo na sasa umeamua kumwambia mtoke wote. umeona uruke ili kupata mpira unaozunguka.
 
3.Unaamini mwanaume ambae yuko interested na wewe ni mwoga, kwa hio umeona urahisishe mambo kwa ajili yenu wote kwa kuchukua jukumu la kumwalika .
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nguvu kubwa inayobadilisha usawa wa jinsia sehemu za kazi, inaonekana kama kumwalika mwanaume ili utoke ingekuwa hakuna tatizo kubwa.
 
Hata hivyo, wewe ni mfanyabiashara unaezunguka labda tuseme hivi, una mafanikio kwa sababu ya juhudi yako. Na hii labda ni sehemu mojawapo ya kujiongeza ili kitu kifanikiwe , si sawa?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Ukweli ni hapana. kwa mapenzi ya kawaida kati ya mwanaume na mwanamke sio rahisi kama hivyo. katika tofauti za kinjia katika mahusiano ni muhimu kuwe na mipaka . labda kama umefikia miaka 40 hapo unaweza ukawa huna aibu ya kumwalika mwanaume kutoka nae.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Katika mbio za wanadamu , wanaume ni wawindaji, huchukua muda kuwinda, ili kupata kitu bora kwa ajili ya familia. wanawake ni kwa ajili ya kulima , kuzaa na kuwatunza watoto. lakini wanaume wanaweza kufanya usafi pia.
 
Kwa hio hii kujiongeza na kujifanya wewe kuwa mwindaji, ni kwa sababu ya tabia zilizoingia kwa wanawake wa siku hizi.

Nina maana kuwa huwezi kumwalika mwanaume , kwa sababu mwanaume hatakuwa huru na wewe, atajiona kama unamwendesha na kumtawala.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Wanaume wa ukweli hufuata mila na desturi – huchagua mwanamke wa kutoka nae na huchukua gharama zote sehemu mnayokwenda.

Lakini kama wewe ndio mlipaji wa kila kitu kule mnakoenda, atakuwa anajua tu kuwa hamtadumu kwa muda mrefu zaidi ya kipindi hicho. utakuwa hapo unamkimbiza taratibu.
 
Wanaume wanaojielewa huwa hawakubali kukimbizwa, Hata kama usawa wa kibinadamu upo sehemu katika maisha yao.

Kwa sababu wanaona ni kinyume na uwanaume wao , kutochukua gharama ya malipo , jukumu lao, ni kama kujidhalilisha duniani.Vingine vyote vinakubalika , vitu vinavyomfanya kuishiwa nguvu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwa kawaida kama umemwalika mwanaume na akaonekana kukubaliana na wewe, pia akakuomba utoke nae tena. kama itatokea hivyo, mwache yeye achukue jukumu la gharama zote, kwa sababu hii ndio njia ya pekee ya kufahamu ili uweze kujenga mahusiano na yeye.
 
Lakini pia kama ulihitaji kumwalika mara moja , ni sawa. kwa sababu huhitaji kitu chochote cha muda mrefu. haina tatizo ni nani atachukua jukumu la malipo.

Lakini kama unatafuta mapenzi, ushauri wangu ulio bora kwako ni kuacha mwanaume akualike kutoka nae.
 
Kitu cha muhimu zaidi, nataka wewe ukifahamu ni kwamba , kama hajakualika kutoka nae , ni kwa sababu hakuhitaji.

Vinginevyo angekualika. ndio, ni rahisi kama hivyo.

Mwanaume huwekeza kwa mwanamke anapohitaji kuuteka moyo wake. hii ndio kusudi la mkimbizaji. ndio maana anakutaka wewe uache kila kitu kwa ajili yake, ili uwepo zaidi. usikivu mdogo tu unampa changamoto kubwa, utamfanya uwindaji wake uzidi na kutaka kukuweka mahali panapostahili.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Usichukulie mzaha kwenye ukimbizaji wake!

mwanaume huangalia mahali ambapo atajisikia ushindi, kwa hio usije uka mkosesha changamoto na ukimbizaji wake.

Ushindi wake utaonekanaje endapo wewe utamwalika kutoka nae?
 
Furaha yake itatoka wapi kama utachukua ushindi wake?

Hakuna hata kimoja hapo kinachosaidia kumuimarisha misuli yake, badala yake , itakuwa ni hali ya kushindana – kitu ambacho KAMWE HAKITAKUONGOZA KWENYE MAPENZI.
 
Back
Top Bottom