Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️
 
Kumekua na hulka ya akina dada, hasa wa kizazi cha leo, akina mama sio sana pindi anaposikia kuwa mume wake amechepuka ataanza kuhisi mambo mengi, kama kujitoa kasoro, au kufikiria nini mume wake amekosa kwake, je hana uzuri wa kumvutia mumewe? Au kaamua kutoka kwa kua anamdharau nk,jibu rahisi ni kwamba unaweza usiwe na kasoro yoyote ile, tena yawezekana mchepuko wa mwanaume wako unaweza ukawa haukufikii wewe kwa lolote,
 
Wanaume kuchepuka ni hulka yao tuu hasa nchi zetu za kiafrika, tena mara nyingi wengi huwa hawana sababu ya msingi ya kufanya hivyo isipokuwa ni "just for new taste" na kuonyesha "identity na prestige" tuu na ndio maana wanaume wengi wanaochepuka huwa hawataki kabisa kuanza kuongea madhaifu ya mkewe kwa mpango wa kando wake, hii ni kuonyesha kuwa anaheshimu nyumbani kwake na hayuko radhi kuharibike.
 
Imekuja kuonekana miaka ya karibuni kuwa ni kikwazo hasa baada ya kuzuka harakati nyingi za "kumkomboa" mwanamke na mambo ya "haki sawa" kwamba kuwepo na nguvu sawa za kimamlaka ndio zimekuja kusababisha migogoro mingi na kutokuelewana miongoni mwa wanandoa siku za karibuni, kwamba baba akichepuka na mama lazima afanye hvyo.
 
Kwa bahati mbaya jamii imekua na hukumu tofauti kwa kosa moja lililotendwa na watu wa jinsia mbili tofauti kwa hyo dada zangu ukiona hari hyo inatokea usishangae sana wala kujiuliza una tatzo gani, kama una kasoro za kawaida zisahihishe ila walio wengi atatoka hata kama huna kasoro, chakufanya chukua hatua stahiki za kuendelea kuokoa mahusiano na kuendelee kumnasihi mwandani wako akumbuke familia na amuogope Muumba wake, wengi hua wanaelewa.

Muhimu: Sihamasishi wanaume kufanya hivyo, haifai.
 
Uhusiano maridhawa katika ndoa ni kitu kinachohitaji kujituma kwa bidii kubwa. Ni kitu kinachohitaji subira, uelewa na upendo kwa pande zote mbili.

Wakati unapenda kumfanya mwenzio kuwa mwenye furaha, kuna mambo kadhaa unayoweza kuyafanya kuhakikisha nawe unapata furaha. Ukweli kama hutofanya mambo haya matano, hutokuwa na zana sahihi zinazokupa furaha katika maisha ya ndoa yako:
 
Kumuamini.
Imani ni ufunguo wa furaha katika maisha ya ndoa. Usipomuamini mwenza wako utaendelea kukosa utulivu na kuwaza kuwa yuko wapi, yuko na nani au anafanya nini. Stress na mashaka utakayoyapata kutokana na wasiwasi na hisia za kuhisi kile anachofanya vitakuondolea furaha yako.

Ili uwe na furaha unatakiwa kuwa na imani, kumuamini. Imani inaweza kuchukua muda mrefu kuijenga, lakini ni kitu nyeti sana. Hakikisha unamweleza mwenzako wasiwasi wako pindi jambo fulani linapokuwa haliko sawa. Inaweza ikawa ni kutoelewa tu, lakini ukiiruhusu shaka ishike hatamu, inaweza kugeuka kuwa tatizo kubwa zaidi. Usiiruhusu shaka itawale maisha yako. Usiiruhusu shaka ndio iongoze maisha yako. Jiamini na umuamini, hiyo ni dawa kiboko
 
Kumpa nafasi.
Kama unataka kuwa na furaha na mumeo hakikisha unampa nafasi, usimbane. Muache ajumuike na marafiki zake au kushiriki mambo ya maana anayoyapenda. Humfanya apate fursa ya kuwa mbali nawe kwa muda fulani na kuongeza nishati mpya ndani ya moyo na akili yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…