Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukweli nikwamba Nuru Na Giza Haviwezi kukaa pamoja. Kwa kuwa Nuru ikiwepo giza hutoweka, na mahali penye Giza hakuna Nuru. Kama wewe unafanya kazi na watu wa aina hii ni ngumu kufanikiwa. Labda kama shirika linahitaji watu waaminifu utaweza kupona. Kumbuka wakati mwingine shirika huhitaji watu wabaya kwa kutaka kujulikana pasipo halali au kukata kazi zifanyike kwa njia watakazo wao.
 
Utafanyaje kama utajua uko mahali penye sumu kama hio? Watu wenye utu wa giza. Ni bora kufanya utaratibu wa kutafuta mahali kwingine, vinginevyo utafanyiwa vibaya , utafanya kazi zako kwa shida. Kama unaweza kucheza mchezo wenye nguvu. cheza na Mungu mwenye nguvu, Simama katika kweli, fanya kazi zako vizuri kila siku. jijengee utu wako vizuri , uwe jasiri, uwe na imani, tafuta maarifa ya kutosha , onyesha upendo. Usiende kushoto wala kulia, baki na Mungu Hapo utashinda.
 
Jitosheleze kazini , vilevile hata katika mahusiano, usiige ubaya, funika ubaya kwa wema. Hukuumbwa na hofu wala woga, kufanikiwa kwako ni lazima, usiteseke na mtu . Uwezo ulionao ni mkubwa huhitaji kuteseka.
 
34034420_366677440403151_5940466084250386432_n.jpg
 
Fahamu kwamba ndizi mbivu ina faida kwenye urembo. Hili ni tunda ambalo lina wingi wa madini ya potassium. Madini haya yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuifanya ngozi yako iwe na muonekano mzuri.

Je wajua kuwa maganda ya ndizi ni tiba ya chunusi? Kama unasumbuliwa na chunusi wala usipate shida kutafuta dawa zenye kemikali . Tumia tunda hili kupata ufumbuzi.


Ili kupata matokeo mazuri, chukua maganda ya ndizi na uyasugulie katika eneo ambalo limeathiriwa na chunusi. Hakikisha unasugua hadi ule weupe unapotea na rangi ya hudhurungi itaanza kutokea. Virutubisho vinavyotoka kwenye maganda hayo ndivyo vinavyokwenda kutibu chunusi na makovu.
Ukifanya zoezi hili angalau mara mbili kwa wiki utapata matokeo mazuri.

Maganda ya ndizi yanaweza kutumika kuondoa weusi kwenye kuzunguka macho. Saga ndizi mpaka ilainike kabisa kisha paka katika eneo unalotaka kuondoa weusi. Kama ngozi yako ni kavu changanya ndizi iliyosagwa na asali. Sugua mchanganyiko huo kisha uuache kwa dakika 15 mpaka 20 kisha nawa kwa maji baridi.

Ndizi inaweza kutumika kama kulainisha ngozi ya miguu pia. Unachotakiwa kufanya, isage ndizi ilainike na kisha uipake kwenye miguu. Kaa nayo kwa dakika 20 kisha nawa kwa maji safi ya baridi. Hii huifanya miguu kuwa laini na yenye kuvutia.
 
Ni vema tukikubaliana na ukweli kwamba hakuna hata mmoja kati yetu ambaye alizaliwa akijua kuwasiliana. Wote tunajifunza, na inabidi mtu kuamua kukubali kujifunza kuwasiliana ili kuwa muwasilianaji bora.

Yamkini ukajiuliza, ni kwanini wengi wetu tunashindwa kuwasiliana vema? Ukweli ni kwamba wengi wetu hatujawahi kufundishwa namna bora za kutuwezesha kuwasiliana vema na pia hatujakubali kujiruhusu kufahamu mbinu bora za mawasiliano yenye ufanisi.
 
Kwahiyo kitu cha muhimu na cha maana kwa sasa ni kama unataka kuyaona mabadiliko ndani yako basi amua kubadilika. Amua leo kuanza safari ya kuelekea kuwa muwasilianaji aliye bora. Zifuatazo ni faida utakazo zipata mara utakapoweza kufanya mawasiliano yaliyo bora na yenye ufanisi:

Mawasiliano bora na yenye ufanisi yatarahisisha maisha yako
Mawasiliano bora na yenye ufanisi yatakupanulia wigo wa kujulikana
 
Mawasiliano bora na yenye ufanisi yatakusaidia kufikisha ujumbe ipasavyo
Mawasiliano bora na yenye ufanisi yatakusaidia kapata matokeo mazuri
Mawasiliano bora na yenye ufanisi yatakupunguzia misongo ya mawazo katika maeneo mbali mbali
 
Baadhi ya mambo ya kuzingatia

1. Jitahidi kuwa mtu wa kuzungumza na sio mtu wa kubishana
Mazungumzo ni kule kuongea kwenye lengo la kufikia lengo au hitimisho fulani wakati mabishano ni kule kuongea ambako kunapelekea mtu au watu kuumizwa kihisia na pia kumtafuta mshindi na mshindwa.
 
Baadhi ya mambo ya kuzingatia

1. Jitahidi kuwa mtu wa kuzungumza na sio mtu wa kubishana
Mazungumzo ni kule kuongea kwenye lengo la kufikia lengo au hitimisho fulani wakati mabishano ni kule kuongea ambako kunapelekea mtu au watu kuumizwa kihisia na pia kumtafuta mshindi na mshindwa.
 
Jitahidi kuwa msikilizaji na tamani sana na wewe kusikilizwa pale inapowezekana.
Wengi wetu tunapenda sana kuongea na sio kusikiliza, hili ni tatizo kwasababu asiye sikilizwa huhisi kuumia sana ndani yake. Kama ambavyo unahisi unahaki ya kuzungumza kwenye hilo jambo unalotaka kulizungumza basi vivyo hivyo unahaki pia ya kusikiliza wakati mwingine anaongea.
 
Kama mtu anaongea na wewe, baada ya yeye kuongea au hata anapokuwa anaonyesha kuchukua muda mrefu zaidi kwenye kuongea muombe akupenafasi na wewe uzungumze ili na yeye akusikilize. Yakupasa kufahamu kwamba kamwe hamtafika popote kwenye hicho mnachokiongelea hatakama ni cha muhimu kwa kiasi gani kama wote mtakuwa mnazungumza kwa wakati mmoja.
 
Jinsi gani ya kuwa msikilizaji mzuri

Sikiliza vema na muelewe mzungumzaji
Elewa kwa ufasaha madhumuni ya kinachozungumzwa
Uliza pale ambapo unaona haujaelewa vema
Fanya tathmini ya kile kilichozungumzwa, kiseme kwa muhtasari na
kwa maneno yako ili kuonyesha kama umekipata sawia
 
Back
Top Bottom