Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UTAFITI: Mpango wa Chakula na Mazoezi Kwa Mgonjwa wa kisukari Ni Tiba Tosha



Kwa mgonjwa wa kisukari anashauriwa kuweza kufanya yafuatayo ili kuweza kupunguza kiwango cha sukari katika mwili wake. Kwani inasadikika ya kwamba kwa mgonjwa wa kisukari anatakiwa kuwa na kiwango cha kati cha sukari katika damu, kwani pindi sukari ikipungua sana (Hypoglycemia) au sukari ikizidi (Hyperglycemia) huwa ina athari kubwa kiafya.
 
1. Kula chakula cha wanga kwa wingi.
Mgonjwa wa kisukari hana masharti ya ajabu kuhusu chakula anachotakiwa kula, kimsingi anaweza kula chakula chochote anachopenda. Kuna mambo matatu ambayo yanabidi kuangaliwa katika kuweka kiwango cha sukari cha mgonjwa kwenye kiwango kinachofaa. Mambo hayo ni:
 
Watalaamu wa afya na mambo ya chakula wanabainisha kwamba chakula kinachotakiwa kuliwa kwa wingi zaidi ni chakula chenye wanga (carbohydrates), kikifuatiwa na mboga na matunda, kisha chakula chenye protini na mwisho ni chakula chenye mafuta (fats).
 
Tunapozungumzia chakula Chenye Wanga hapa tuna maana chakula ambacho kinapatikana zaidi kati mboga za majani, nafaka, matunda pamoja na maziwa ya mgando. Wataalamu wanasisitiza kula chakula hiki cha wanga kwani aina hiyo ya vyakula husaidia katika kuzalisha glucose ambazo husaidia kuweza kujenga nguvu za mwili na kuupa nguvu mwili
 
Ugonjwa Wa Chango La Uzazi - (Mke / Mume)



Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume. Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni. Kwa mfano :- mume, hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo. Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo. Maumivu hayo hupelekea mtu (mume/mwanamke) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi.
 
DALILI ZAKE

Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana.
Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha.
Ni vigumu kumpa mimba mwanamke.
 
Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:-

Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi
Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika
Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi
Kupatwa hasirakali/ jazba anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi.
Kujisikia uchovu mkubwa anapokaribia siku zake za hedhi.
Kupata mchubuko kwenye mapaja na sehemu za uke.
Kuchukia kushiriki tendo la ndoa
Kupata uvimbe kwenye kizazi
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi
 
Madhara yake kwa mwanamke


Kwa mwanamke ni vigumu kupata mimba
Mwanaamke anaweza kuwa tasa kabisa
Kuingia na kutoka kwa mimba
Kuwa na hamu ya tendo la ndoa lakini hafikii kileleni
Kuwa na uke mdogo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…