Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HATUA makundi imeshapita na sasa ni mtoano, ukipiga anakwenda nje kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko Russia. Wakati timu 32 zikipungua na kufikia 16 bora huku nyingine mbili zilitarajiwa kutupwa nje ya michuano hiyo kuanzia jana Jumamosi, kuna mastaa hao wameonyesha kiwango bora kinachowafanya waanze kuhusishwa na tuzo ya mchezaji bora wa fainali hizo za Kombe la Dunia 2018, yani Golden Ball.
 
Kwenye fainali zilizopita, washindi waliwahi kuwa Lionel Messi, Diego Forlan na Zinedine Zidane, ambapo wakati wananyakua tuzo hiyo timu zao hazikuwa mabingwa, hivyo kuwa mchezaji bora kwenye fainali za Kombe la Dunia hakuna maana hadi ubebe ubingwa, kikubwa ni kucheza kwa kiwango bora kinachoifanya timu yako kufanya vyema uwanjani. Hii ndiyo orodha ya wakali watano wanaotajwatajwa kwamba huenda wakahusika kwenye tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia 2018 huo Russia.
 
Luka

Modric

Kiungo huyo wa Croatia, Luka Modric amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia. Kiwango bora cha Modric kimeifanya Croatia kutinga mechi zote tatu za hatua ya makundi. Akisema sambamba na Ivan Rakitic kwenye sehemu ya kiungo wawili hao wameunda kombinesheni matata kabisa kutesa kwenye soka hilo la kibabe. Modric ni mmoja wa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa fainali za Kombe la Dunia huko Russia.
 
Harry Kane

Straika, Harry Kane amecheza mechi mbili tu kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia na kufunga mabao matano yanayomfanya kuwa kinara kwa kutupia katika fainali hizo. Lakini, hiyo ilikuwa kabla ya mechi za jana, ambapo Cristiano Ronaldo mwenye mabao manne alitarajia kucheza na kama atakuwa amefunga basi atakuwa ameshamfikia Kane. Kwenye fainali hizo za Russia, Kane anafukuzia tuzo mbili, Kiatu cha Dhahabu na Mpira wa Dhahabu kwa maana ya kuwa mchezaji bora wa Kombe la Dunia.
 
Cristiano Ronaldo

Staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo alipiga mabao matatu kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Hispania, kisha akaja kufunga bao pekee wakati Ureno ilipoichapa Morocco kwenye mechi ya pili ya kundi lao. Usiku wa jana Jumamosi, Ronaldo alikabiliwa na mtihani mwingine mgumu wa kuwakabili Uruguay kwenye mechi ya hatua ya 16 bora inayohusu mtoano.
 
Lakini, kwa kiwango alichokionyesha staa huyo kwenye mechi za makundi tu zimemfanya kuwa na nafasi ya kuwamo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa fainali hizo za Russia.
 
Coutinho alifunga bao maridadi kabisa kwenye mechi ya kwanza, kisha akaja kufunga tena kwenye mechi ya pili, kabla ya kutoa asisti matata kwenye mechi ya tatu ya hatua ya makundi huku Brazil ikitinga raundi hiyo ya 16 bora bila ya presha. Kiwango chake hicho kwenye hatua ya makundi, imemfanya Coutinho kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaweza kuibuka na kubeba tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2018.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…