Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Eden Hazard

Kama kuna fainali za Kombe la Dunia ambazo Eden Hazard ana nafasi kubwa ya kutamba licha ya kuwapo kwa mastaa wa maana kabisa kama Eden Hazard na Cristiano Ronaldo basi ni hizi za Russia. Hazard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kwenye kikosi cha Ubelgiji, huku umahiri wake ukiifanya timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia bila ya wasiwasi wowote, ikishinda mechi zote kwenye kundi lake. Hazard ni mmoja wa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kuchuana kwenye kuwania Mpira wa Dhahabu wa fainali za Kombe la Dunia huko Russia.
 
Nahodha na mshambuliaji mahiri wa Misri, Mohamed ‘Mo’ Salah, alijikuta katika wakati mgumu, baada ya Alhamisi usiku kuvamiwa na kundi la vijana waliotaka kumuona.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa BBC, Shaimaa Khalil, habari za Salah kuwepo kijijini Nagrig nje ya jiji la Cairo, kwa ajili ya mapumziko zimevujishwa na mmoja wa ndugu zake wa karibu kupitia mtandao wa Facebook.
 
Baada ya kupata taarifa hizo za kuwepo kwa Mo Salah kijijini mashabiki wake walikwenda kwa madhumuni ya kumuona, huku wengine wakitaka kuzungumza naye kupata ufafanuzi na ikibidi wamsihi abatilishe uamuzi wake wa kutaka kustaafu kuichezea Misri.
 
Licha ya mshambuliaji huyo kujitokeza na kuwasalimia mashabiki hao huku akisaini fulana na vijitabu vyao, hakuweza kuwamaliza kwani kila nukta moja ilivyopita ndivyo umati huo ulivyoongezeka na kulazimika kuitwa Polisi kuja kusaidia kuwaondoa.
 
Polisi hawakufanya haraka kuwaondoa mashabiki hao bali waliimarisha ulinzi, lakini baada ya kuona usiku unazidi na dalili za watu kupungua hakuna iliwabidi wazungumze na mshambuliaji huyo na kumtaka aingie ndani ili wao wapate nafasi ya kuwaondoa mashabiki kwa nguvu na wakafanikiwa.
 
Mo Salah ambaye amepewa uraia wa heshima wa Chechnya, amekuwa katika kipindi kigumu kutokana na jeraha la bega alilolipata katika mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya, kumfanya ashindwe kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa kiwango chake hivyo kuinyima Misri mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…