Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huko Japan nako kuna wanaume wa hizi kazi, kama Keisuke Honda, Takashi Inui na jembe mwenyewe, mzee wa kugawa mipira, Shinji Kagawa. Tangu 2010, Keisuke Honda amefanikiwa kufunga mabao zaidi ya manne na kutoa asisti tatu katika mabao saba za Japan katika mechi 10 walizocheza. Hatari!
 
WACHEZAJI HATARI

Belgium - Romelu Lukaku

Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku sio mtu wa mchezo mchezo. Mabeki wanapata tabu sana anapokatiza mbele yao. Mpaka sasa ana mabao manne, goli moja nyuma ya Harry Kane wa England. Mbali na Cristiano Ronaldo na Edison Cavani, Lukaku naye amefanikiwa kufunga magoli akitumia miguu yote miwili na kichwa.
 
Japan - Takashi Inui

Kiungo mshambuliaji wa Eibar, Takashi Inui, mwenye umri wa miaka 30, hayupo katika daraja la akina Kagawa na Honda, lakini amekuwa mmoja wa watu hatari sana katika kikosi cha Samurai Blue, kwenye Kombe la Dunia. Ana kasi, nguvu.na uwezo mkubwa wa kupiga mabao ya hatari.
 
Which one of the following do you use
anonymous poll

Liquor (Pombe) – 139
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106] 33%

I don't use either – 121
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106] 28%

Weed(Bangi) – 115
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106] 27%

Cocaine – 22
[emoji106] 5%

Sheesha – 15
[emoji106] 4%

Heroine – 14
[emoji106] 3%

[emoji186] 426 people voted so far.
 
Kila mtu alishuhudia alichotaka kukishuhudia. Kwa namna awezavyo kila mtu aliushangilia ushindi wa Uruguay dhidi Ureno. Ilikuwa ni burudani ya aina yake. Nafsi zilifurahi kwa kweli. Uruguay 2-1 Ureno.
 
Mwanaume wa shoka Edison Cavani, aliamua kuwaua Wareno mwenyewe bila kuomba msaada. Mabao mawili yalitosha kumpa Cristiano Ronaldo kibali cha kimfuata Lionel Messi uwanja wa ndege. Ilikuwa ni aibu.
 
Kwa wale ambao hawakubahatika kufika Fisht, huko Sochi, kilomita 2,059 kutoka Kazan, ni kwamba Uruguay walitisha sio kidogo. Katika dakika ya saba, Edison Cavani alipiga krosi ndefu iliyomkuta Luis Suarez.
 
Bila kufanya ajizi wala choyo, akawala chenga mabeki kadhaa wa Ureno, kabla kuachia krosi kurudi upande wa kushoto wa uwanja, ukamkuta Cavani, aliyepiga kichwa safi na kumuacha kipa wa Ureno, Rui Patricio, akiwa hana la kufanya zaidi ya kushangaa shavu zake zinavyotikisika!
 
Baada ya hapo walichachamaa wakapata bao la kusawazisha lililofungwa na Pepe, katika dakika ya 55, kabla ya Cavani kukwamisha bao la ushindi katika dakika ya 62. Baada ya hapo likafuata tukio litakalokumbukwa miaka na mikaka.
 
Moyo wa Cristiano Ronaldo ukauthibitikia Ulimwengu mzima. Namheshimi kwa hili. Wanasema muungwana hana alama, ila kwa hili, Ronaldo aliionesha dunia yeye ni nani. Tutamkumbuka kwa hili!

Bila kujali kuwa Cavani ndiye aliyewaua, bila kinyongo, Cristiano Ronaldo alionesha kuguswa. Wakati dunia ikimtegemea kufanya jambo, kuisaidia Ureno, Ronaldo aliamua kumsaidia Cavani. Kwake utu ulikuwa kitu cha muhimu wakati ule na sio vingine.
 
Ni hivi, Edison Cavani aliumia muda mfupi baada ya kufunga bao la pili, ikabidi aondoke uwanjani. Sasa wakati anaondoka, akiwa anachechemea huku akionesha dhahiri kuwa katika maumivu makali, Ronaldo aliamua kumsaidia akimshika na kumkokota hadi nje ya uwanja.
 
Hiki kitendo kilimgusa kila mtu, nakumbuka pale bandani kwa masai muuza kahawa, jinsi watu walivyotulia tuli. Hatukuamini macho yetu. Dunia ilisimama kwa heshima ya mreno yule. Licha ya Ureno kubanduliwa, Cristiano Ronaldo ameacha gumzo katika fainali ya mwaka huu, mitaa yote ya Urusi itazidi kumkumbuka, Wauruguay wanamheshimu hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…