Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jinsi ya kujenga hisia za furaha
Hatua ya kwanza katika kujenga furaha ni kuchunguza jinsi maisha yako ya nyuma yalivyokuwa. Jiulize kama katika miaka iliyopita maisha yako yalikuwa ya furaha au hapana.

Kama hayakuwa ya furaha jiulize ni mambo gani uliyoyafanya au unayoyafanya sasa hata yakupe au yakunyime furaha? Njia hii atakufanya utafakari kwa kina jinsi hali ilivyokuwa na kilichosababisha hali hiyo.
 
Uchunguzi wa kina wa hali ilivyokuwa na sababu zake itakusaidia kutambua jinsi ya kubadilisha hisia na mtazamo wa maisha yako ya sasa.

Wala haitakuwako hoja ya kuhuzunika kwa yale yaliyopita ila kuyatazama maisha yajayo huku ukijiandaa kuyachukulia kama yalivyo na kufanya juhudi za pekee kuhakikisha haitokei hisia ya yale mabaya yaliyotokea zamani.
 
Jambo ambalo hutokea mara kwa mara ni kuweka lawama kwa watu wengine kwa changamoto zinazotokea maishani mwetu.

Mtu anapojitambua udhaifu au makosa yake siyo rahisi kujenga hisia potofu kuwa matatizo yake yanasababishwa na watu wengine. Mara nyingi tumewahukumu watu wengine kutokana na mtazamo hasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…