Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BMjIwWMgVR1.jpg
 
.J. Newberry mtaalamu wa masuala ya tabia aliwahi kusema kuwa ni kazi rahisi kumtambua mtu muongo endapo utajifunza mbinu za kumfahamu, lakini akaongeza kuwa ni vigumu sana kumnasa muongo kwa njia za kubahatisha. Huu ni ukweli kwamba, wengi huongopewa na wapenzi wao na kujikuta kwenye utata wa kuamini wanachoambiwa na wenza wao ni cha kweli au uongo.
 
Nimechelewa kwenye foleni, nilikwenda kumtazama mama mgonjwa” Maelezo haya ukiyaangalia unaweza kuamini, lakini pengine unapolinganisha na muda aliofika mpenzi wako nyumbani unabaki kwenye utata, kama kweli alikwenda kumuona bibi yake au alikwenda kufanya usaliti? Kwa kutambua hilo, mada hii inakuja na njia 10 za kumtambua mtu anayeongopa.
 
MNASE KUPITIA SHUKU
Njia namba moja ya kumtambua mtu muongo ni shuku. Wataalamu wanasema kuwa kama mlio wa bunduki utatokea na mtu akakimbia bila hata kutazama ulikotoka ujue mtu huyo ana uongo ndani ya nafsi yake na kinachomkimbiza si mlio bali woga wake.
Kwa maana hiyo kama ataingia mumeo au mkeo ndani na ghafla akaonesha kushtushwa na uwepo wako jua kuwa ana uongo moyoni au akiacha kufanya jambo fulani kwa kuingia kwako tambua kuwa kuna jambo la uongo ambalo linamuongoza. Muulize vizuri.
 
MUULIZE ASILOTARAJIA
Swali la kushtukiza lisilotarajiwa linaweza kukusaidia kumtambua mtu muongo anasema Sir Walter Scott kutoka Uingereza ambaye ni mshauri wa masuala ya jamii. Anasema waongo wengi wanapodanganya huwa wametayarisha majibu yao, kupitia maswali wanayotarajia kuulizwa. Kwa mfano akisema, kulikuwa na foleni njiani anakuwa na maeneo ameyaweka tayari. “Yaani kutoka Kigogo pale njia panda magari yalikuwa hayatembei kabisa.”
 
Back
Top Bottom