Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sasa ili umnase muulize jambo ambalo haliko kwenye mpangilio wa uongo wake, kwa mfano hivi magari ya kutoka sehemu fulani yanayopitia hapo Kigogo siku hizi yanakatiza wapi kupisha foleni?” Utashangaa anaanza kutoa macho huku akitafuta jibu wakati inawezekana ulichomuuliza si cha kweli, lakini kwa sababu anadanganya atataka kukupa jibu, ujue huyo ni muongo.
 
MBANE KUHUSU MAELEZO YAKE
Waongo wengi huwa hawana kumbukumbu za zaida, wanapodanganya walikuwa wanakunywa baa fulani husahau kutunza kumbukumbu hizo na kujikuta baadaye wanataja kitu kingine au wakakana kutoa maelezo kama hayo. Hivyo unapokuwa na mtu muongo kariri maneno ya kwanza na kisha umuulize baadaye ukitaka ufafanuzi utashangaa yote yameshayeyuka kichwani kwa muongo na kubaki akikutazama asijue la kufanya.
 
MTAZAME MUONEKANO WAKE
O'Sullivan aliwahi kusema watu waongo huwa na sura tofauti wanaweza kucheka wakati nyuso zao zinalia. Au wakati mwingine kupenda sana kupata msaada wa nguvu za mwili kupitia kuchezea vidole au kushika shika majani.
Kwa mfano unapokuwa unamtongoza mwanamke ukiona anaacha kukuangalia na kuanza kuchezea vidole au kijiti jua amekukubali hata kama kinywani ataendelea kukataa. Watu waongo nao huficha uongo wao kwa njia hizo. Hivyo unaweza kumtambua muongo kwa kutazama muonekano wake wakati akiongea na wewe.
 
MTISHE KWA ADHABU
Njia nyingine ya kumtambua mtu muongo, ni kumtisha kwa kuchukulia hatua za kustahili na kosa lake. Mapema tu katika mazungumzo yako unaweza kumwambia hivi: “Kwa kuwa umenichosha kwa tabia zako leo lazima niujue ukweli na nitahakikisha unachosema kina ukweli” Si unasema umechelewa kazini, mimi niko tayari kumpigia simu bosi wako kumuuliza” Baada ya kumpa maneno kama hayo ya vitisho anza kumuuliza, utaona anavyokuwa mpole maana anajua akikutajia alikwenda kwa rafiki zake utataka kwenda huko au kumpigia simu hivyo atalazimika kusema ukweli.
 
TAMBUA KUPITIA ISHARA ZA MACHO

Paul Ekman mwanasaikolojia kutoka Chuo cha California Medical School cha San Francisco, anasema mawazo yanayokuwemo ndani ya moyo wa mwanadamu hujulikana kupitia uso wake. Mwenye huzuni moyoni hutambulika usoni hata kama mhusika atakuwa akicheka kama nilivyosema na kadri ukweli wa jambo unavyozidisha msukumo moyoni uso nao hubadilika kulingana na ukweli huo, hata kama mtu atakuwa ameshikilia msimamo wake wa kukataa kukiri ukweli. Msome mtu kwa kumtazama usoni na usimpe nafasi ya kutazama pembeni.
 
ANGALIA MKANGANYIKO
Njia nyingine ya kumtambua mtu muongo ni kumchunguza kuhusu mkanganyiko wa maelezo yake na ishara anazozitoa kupitia kichwa au mikono yake. Mtu muongo unaweza kumuuliza jambo kichwa kikakataa, maelezo yake yakakubali. Hivyo ni vema kufuatilia uhusiano wa maneno, ishara za mwili, sauti yake na vitendo vyake. Ukiona vinapishana tambua kuwa huyo ni muongo.
 
KUHUSU HALI YAKE YA KAWAIDA
Mtu muongo unaweza kumtambua kupitia kawaida yake, ikiwa mpenzi wako ni mtu wa furaha anapokutana nawe lakini ikatokea bila sababu yoyote anapoteza furaha na kutoona umuhimu wako tambua kuwa ana uongo moyoni mwake unamsumbua, ni vema ukamuuliza.
 
MAELEZO MENGI
Wapenzi wenye uongo huwa na maelezo mengi, utakuta kitu kidogo tu cha kujibu ndiyo au hapana yeye anatoa maelezo mengi yasiyokuwa na msingi. Ukiona hivyo tambua kuwa mpenzi wako ana tabia ya uongo na kwamba anarefusha maelezo ili kuujenga uongo wake uonekane ni kitu cha kweli.
 
USIPUUZE UKWELI
Pamoja na mambo yote tuliyojifunza kuhusu waongo, si vema kuyapuuza yote kwa sababu tu umebaini kuwa mtu fulani ni muongo, lazima ya ukweli yapewe nafasi yake. Kwa mfano muongo anapoeleza jambo la kweli muunge mkono, ili kumfanya mwenyewe atofautishe ukweli na uongo anaopika. Ukikataa yote atakuona wewe ndiyo muongo kwa vile utakuwa umekataa mambo ya ukweli aliyokuambia.
 
Hapana huyu si mume wangu, ila niko naye tu kwa ajili ya kujipumzisha” “Aah, yule msichana wa jana usiku? Siyo mchumba wangu, ‘nazuga’ naye tu, mchumba wangu yuko masomoni.” “Hapana yule ni ‘demu’ wangu mwingine, mwenyewe amesafiri” Hizi ni baadhi ya kauli ambazo watu huzitaja kuelezea namna wanavyowachukulia wapenzi wao.
 
Je ulishawahi kujiuliza wewe ni nani kwa mpenzi wako, ni wa ndoa au wa kustarehesha mwili?
Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wengi wanafahamu mapema zaidi jibu la swali hili kutokana na kanuni za kimapenzi kuwapa nafasi ya kuanzisha uhusiano, tofauti na wanawake hasa wa kiafrika ambao husubiri kutongozwa.
 
Hii ina maana kuwa, wanaume hutambua mapema kuwa mwanamke wanayemtafuta kwa wakati huo huwa ni wa kustarehesha mwili, wakiamini kuwa wa kuoa wanaye au walishamchagua tayari, ingawa hutokea mabadiliko, lakini si makubwa. Tatizo hili limekuwa likiwatia simanzi wanawake wengi ambao mwanzo hudhani kuwa wamepata wanaume wa maisha, kumbe wanakuwa ni wale wanaohitaji starehe tu.
 
Inaumiza pale unapomchagua msichana kwa lengo la kumuoa au mvulana wa kukuoa na kujikuta umekuwa mtu wa kumtosheleza mwili na kuachwa njia panda. Hivyo basi ili watu wasiumizwe na hili wanatakiwa kujua mapema wanaume/wanawake walionao ni wa ndoa au ni wa kustarehesha mwili? Siku zote sifa za mwanaume/mwanamke wa starehe ni tofauti na wa ndoa.
Utofauti huo upo hata katika umuhimu. Hivi kama una mwanaume ambaye ni kwa ajili ya kukukata kiu huku ukitambua kuwa ana mwanamke mwingine utakuwa na wivu naye wa nini wakati unajua fika wewe ni chaguo la pili? Vivyo hivyo kwa mwanaume. Nadhani utakachojali wewe ni kupatikana kwa huduma yako, likiwemo suala la kupelekwa viwanja na kulishwa chipsi kuku.
Lakini linapokuja suala la ndoa wivu ni lazima na yote haya yanatambulika kwa mtu atakayekuwa na uelewa wa mapema kuhusu mpenzi wake.
 
Kuna faida nyingi za kujua hili mapema, moja wapo ni kuandaa ramani ya kukufanya ufikie lengo lako. Ikiwa mwanaume uliye naye ni wa ‘kuchuna’ lazima afuate ramani ya kuchunwa anapokwepa, abanwe. Na kwa mwanamke wa kuoa naye vivyo hivyo.
Unapokuwa na mpenzi, jambo la kwanza la kufahamu ni hilo la kujua nafasi yako ni ipi kwake? Ukishatambua unachotakiwa ni kuandika ramani ya penzi lenu na kuisimamia. Kwa mfano mwanaume uliye naye akiwa ni wa ndoa, kaeni mpange lini mtaoana, malengo yenu ni yepi, mnatakiwa kufanya nini kuelekea huko, kama ni kutambulishana kwa wazazi, lisiwe ni suala la kusubiri liwe ni la lazima kwa sababu ramani inaelekeza hivyo.
Aidha kama mwaume ni wa kustarehesha, naye awekewe ramani yake, kila wikiendi lazima atoe pesa za kustarehe, awe tayari kwa kuwa pamoja, atoe vocha, alipe kodi ya nyumba na yote yanayohusu jukumu lake asipofanya, anakuwa amepoteza sifa.
 
Jambo linalosikitisha siku hizi ni kuona watu wanakutana sokoni, shuleni na kupeana mapenzi bila kuwa na ramani ya kufuata aidha kuelekea kwenye ndoa au kustareheshana, matokeo yake ni mivurugano ambayo huwaliza wengi.
“Kaniacha kwenye mataa wakati nilikuwa namtegemea kabisa kuwa atanioa” Mtu anayesema hivi ukimuuliza mliwahi kupanga kuoana? Anabaki kimya, lakini kishachezewa miaka mitano mizima na hakuwahi kugutuka kuwa jamaa hafuati ramani ya ndoa.
Jamani ni vema tukawa wazi kwenye mapenzi na uwazi huo utajulikana kwa ramani. Uliyenaye ili umtambue kuwa ni wa ndoa mpe ramani yake, aende kwenu akajitambulishe, akupeleke kwao, akutunze na kukupa kipaumbele kama mke, ukiona hataki kukufanyia hayo tambua huyo ni wa starehe unachotakiwa ni kumtayarishia ramani yake ya kuchunwa kisawa sawa ili upate faida na usije kujuta atakapokuacha au kumfumania.
 
Mimi huwa nashangaa kuona baadhi ya wanawake wanakuwa na wivu hadi kwa waume za watu wakati wanatambua kuwa hawawezi kuolewa, na wao ni changuo la pili. Shida yote ya nini ukiwa unataka ukawe mke mwenza, andaa ramani yako na jamaa aifuate usikae ukidhani jambo litatokea kama mvua . Mwisho niwaonye watu wanaoanzisha mapenzi mashuleni hawa lazima wawe na ufahamu kuwa mapenzi ya aina hiyo mengi huwa ni ya kustareheshana tu na mwisho wake huwa ni baada ya kumaliza shule.
Tena ni vigumu kuyawekea ramani mapenzi ya kishule shule kwa vile wote huwa katika safari ya kutafuta maisha ambayo mwisho wake huwa hayajulikani. Ni vema kusoma kwanza kisha baada ya kupata mwanga wa maisha ndipo suala la mapenzi likatazamwa kwa upana, vinginevyo ni kuchezeana na kuharibiana maisha tu.
 
Back
Top Bottom