Kuna faida nyingi za kujua hili mapema, moja wapo ni kuandaa ramani ya kukufanya ufikie lengo lako. Ikiwa mwanaume uliye naye ni wa ‘kuchuna’ lazima afuate ramani ya kuchunwa anapokwepa, abanwe. Na kwa mwanamke wa kuoa naye vivyo hivyo.
Unapokuwa na mpenzi, jambo la kwanza la kufahamu ni hilo la kujua nafasi yako ni ipi kwake? Ukishatambua unachotakiwa ni kuandika ramani ya penzi lenu na kuisimamia. Kwa mfano mwanaume uliye naye akiwa ni wa ndoa, kaeni mpange lini mtaoana, malengo yenu ni yepi, mnatakiwa kufanya nini kuelekea huko, kama ni kutambulishana kwa wazazi, lisiwe ni suala la kusubiri liwe ni la lazima kwa sababu ramani inaelekeza hivyo.
Aidha kama mwaume ni wa kustarehesha, naye awekewe ramani yake, kila wikiendi lazima atoe pesa za kustarehe, awe tayari kwa kuwa pamoja, atoe vocha, alipe kodi ya nyumba na yote yanayohusu jukumu lake asipofanya, anakuwa amepoteza sifa.