Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni Herufi zinazoonekana katika eneo la mnara wa mtandao katika vioo vya simu zetu ni vifupi vya vizazi (Generation) vya mtandao husika na kwa sasa tuna4G, H+, H, 3G, E (Edge), G (Gprs) na kwa wale watumiaji wa Blackbery kuna alama ya BB kama utakuwa unatumia Blackberry Internet Service maarufu kama BIS. Tunatumia data katika kutuma na kupokea barua pepe, kusikiliza na kupakua, video pamoja na picha mtandaoni,
 
Hivi vyote ni vizazi vya Wireless Network (mtandao usiotumia waya) na tofauti kubwa ni kasi ya kupandisha na kupakua data (uploading and downloading speed). Teknolojia hizi hutegemea sana aina ya simu, na kampuni ya simu inayotoa huduma ya mtandao. Kwa mfano, unaweza ukawa na simu yenye uwezo wa kukamata 4G ila mtandao unaotumia ukawa hautoi huduma hii, hiyo inakuwa sawa na kuwa na boti nzuri yenye kasi alafu unaishi nayo jangwani.
 
1. GPRS (General Packet Radio Service)

Hiki ni teknolojia ya kwanza katika kizazi cha pili cha network, 2G (Second Generation), teknolojia hii ina uwezo wa kasi ya kupakua (download speed) mpaka 171Kbps (Kilobits per second) kama kasi ya juu kabisa ya kupakua. Nchini teknolojia hii ilikuwepo sana kipindi cha miaka ya 2000 wakati mitandao ya simu za mkononi ilipoanza kuingia kwa kasi.
 
2. EDGE (Enhanced Data GSM Evolution)

GPRS na EDGE vyote ni vizazi vya 2G ila EDGE ina kasi kubwa zaidi ya kupakua (download) ukilinganisha na GPRS. EDGE na GPRS zikiunganishwa huwa zinaitwa 2.5G Networks na inakuwa na kasi zaidi. Hapa nchini kwetu kabla ya mwaka 2014 mitandao karibia yote ya simu ilikuwa inatoa huduma hii, na huwa inawakilishwa na heri E au EDGE katika mnara wa network.
 
3. 3G (Third Generation Network)

Kuja kwa 3G kumefanya kuangalia video mtandaoni iwe rahisi au kupiga simu za video, ni mtandao wenye kasi ya wastani na karibia mitandao yetu yote ya simu inatoa huduma hii kwa sasa hasa maeneo ya mijini. Mtandao huu una kasi ya kupakua mpaka 3.1 Mbps na ulianza kutumika rasmi mwaka 2001.
Kama unakumbuka vodacom ndio walikuwa wa kwanza kuleta teknolojia hii hapa nchini
 
4. HSDPA (High-Speed Down-Link Packet)

Hiki bado ni kizazi cha tatu cha mtandao (3G) kilichoongezewa nguvu na kuwa na kasi ya kupakua mpaka 14Mbps na muda mwingine hufahamika kama3.5G . Mara nyingi kwenye simu zetu huwa inawakilishwa na herufi H, na kama nitakua sikosei Airtel walikuwa wa kwanza kujinadi kwa teknolojia hii hapa nchini.
 
5. HSPA+ (Evolved High-Speed Packet Access)

HSPA+ ni muendelezo wa HSPA(HSDPA&HSUPA), ni mtandao wenye kasi zaidi na ni mwanzilishi wa kizazi cha nne cha mtandao (4G). HSPA+ inauwezo wa kupakua mpaka wastani wa 168Mbps kasi kubwa zaidi ya vizazi vyote vilivyopita na huwa inawakilishwa na H+ katika simu zetu.
 
6. 4G LTE (Long Term Evolution)​

LTE ni kizazi cha 4 cha mtandao (4G) kinachosapoti kustream (kuangalia mtandaoni) video za HD (High Definition) au video zenye ubora wa juu kabisa kwa kuwa teknolojia hii ina kasi mpaka ya 299.6Mbps kasi kubwa zaidi kwa sasa. Mitandao kama Smile na Tigo kwa sasa wameshaanza kutoa huduma hii kwenye baadhi ya maeneo nchini.
 
6. 4G LTE (Long Term Evolution)

LTE ni kizazi cha 4 cha mtandao (4G) kinachosapoti kustream (kuangalia mtandaoni) video za HD (High Definition) au video zenye ubora wa juu kabisa kwa kuwa teknolojia hii ina kasi mpaka ya 299.6Mbps kasi kubwa zaidi kwa sasa. Mitandao kama Smile na Tigo kwa sasa wameshaanza kutoa huduma hii kwenye baadhi ya maeneo nchini.
 
Kampuni ya kutengeneza simu ya Samsung Electronics yenye makao makuu yake nchi Korea Kusini tayari wameanza kufanya majaribio ya kizazi cha tano cha mtandao, 5G japo haijatangaza rasmi lini teknolojia hiyo itaingia mtaani.
 
Tunapozungumzi Packets hasa katika teknolojia hizi za kupakua na kupandisha data mtandaoni tunamaanisha kuvunjwa vunjwa kwa kile kitu unachokituma mtandaoni katika vipande vidogo vidogo ile viweze kutumwa au kupokelewa kwa urahisi.
 
Naamini ni wengi wanaomiliki simu za kisasa ‘smartphones’ ambazo zinaendana na teknolojia ya sasa iliyozidi kurahisisha maisha ya mwanadamu kupitia simu hiyo ya kiganjani. Lakini yawezekana si wote ambao wanaifahamu ‘smartphone’ ya kwanza kuingia sokoni.
 
Back
Top Bottom