Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye kiungo nguli, Andres Iniesta, ametangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya kucheza kwa mafanikio katika kikosi cha Hispania.​

Moja ya mafanikio yake ni kuipa Hispania ubingwa wa Kombe la Dunia, alipofunga bao pekee katika muda wa nyongeza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi.

Kiungo huyo ambaye tayari amewaaga mashabiki wa Barcelona aliyoitumikia katika maisha yote ya soka la ushindani, amejiunga na Vissel Kobe inayotumia Uwanja wa Kobe Wing nchini Japan.
 
Anasema huzuni kubwa moyoni mwake, lakini hana namna lazima atimize ahadi ingawa ni uamuzi mgumu ambao hakuwahi kufanya katika maisha yake ya soka.

Hakuna namna yoyote unaweza kumuandika Iniesta katika kurasa moja au mbili za gazeti, lakini kwa uchache haya ni baadhi ya mambo ya kukumbukwa aliyofanya katika medani ya soka akiwa mmoja wa viungo bora waliowahi kutokea duniani.

Katika maisha yake yote ya soka, Iniesta amecheza Barcelona, anaondoka huku mchango wake kwa timu hiyo ukiwa unahitajika.
 
Umuhimu wake ulidhihirika katika mchezo wa juzi, alipoingia akitokea benchi dhidi ya Russia ambapo alibadili sura ya mchezo na Hispania ilicheza kwa ustadi.

Iniesta ndiye aliyechangia Hispania kuvunja rekodi ya mwaka 1966 ya kucheza pasi 1,029 katika mchezo huo waliolala mabao 4-3 kwa penalti, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120.
 
Mambo 30 kuhusu Andres Iniesta:

1. Aliipa Hispania ubingwa wa Ulaya 2008.

2. Alichaguliwa kiungo bora wa Fainali za Ulaya 2008.

3. Aliteuliwa kwenye kikosi bora (Best XI) 2008.

4. Bao lake liliiua Uholanzi na kuipa Hispania ubingwa wa Dunia 2010.

5. Alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo katika fainali zilizochezwa Afrika Kusini.
 
6. Mtu wa mwisho kustaafu kati ya waasisi wa ‘tik-tak’, akiungana na Xavier Hernandez.

7. Ameitumikia Hispania miaka 12, tangu mwaka 2006 hadi 2018.

8. Maisha yake yote amecheza soka Barcelona.

9. Ameichezea Barcelona mechi 442 na amefunga mabao 35.

10. Amecheza mechi mbili timu ya Taifa ya Jimbo linalotaka kujitenga na Hispania la Catalunya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…