Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

N'NGOLO KANTE
Akiwa kwenye ligi ya ipielo na timu yake ya Chalsea kazi yake kubwa ni kukaba. Kocha Didier "didi" Deschamps amemkabidhi dhamana hiyo hiyo huko Russia. Kante anawafanya viungo waliosheheni kwenye kikosi cha ufaransa akiwemo Paul Pogba kucheza bila presha na hivyo kuwasha taa za tahadhari huenda taifa hilo la Ulaya lililosheheni wafrika kuliko wazungu wenyewe huenda wakarudi Paris wakiwa na mwali anayegombewa huko Russia
 
Alisema hii ni mara ya pili kwa baba yake kutekwa katika kipindi cha miaka saba, jambo linalompa wasiwasi na kuitaka serikali kuimarisha ulinzi.

Baba yake mzazi Michael Obi alitekwa Juni 26 mjini Enugu akiwa kwenye gari yeye na dereva wake na waliachiwa huru Jumatatu hii baada ya mwanae huyo kumlipia kikomboleo.
 
Chama cha Soka cha Ujerumani, kimebainisha kuwa Joachim Low, ataendelea kuinoa timu ya Taifa licha ya kufanya vibaya katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia.
Low mwenye miaka 58 alianza kuinoa Ujerumani mwaka 2006 na aliiongoza Ujerumani kwa mafanikio makubwa akiipa ubingwa wa Dunia 2014 na ule wa Ulaya 2016.
 
Hata hivyo katika fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea Russia, Ujerumani imeng’oka katika hatua za makundi ikishinda mchezo mmoja na kupoteza miwili ya kundi G.
Ujerumani haijawahi kutolewa kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1938, hivyo matokeo mabaya ya mwaka huu yalizusha midajala kuhusu hatima yake.
 
Hata hivyo chama cha soka kimesema Low ataendelea kuinoa timu ya Taifa hadi mwisho wa mkataba wake utakaomalizika mwaka 2022.
“Ninayo furaha sana kuona ninaendelea kuaminiwa na chama cha soka mimi ninaomba mashabiki wote wa soka wandelee kutupa ushirikiano,” alisema Low.
 
Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery, jana Jumanne aliongoza mazoezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza tangu asaini kuinoa akichukua nafasi ya Arsene Wenger.
Emery aliongoza mazoezi hayo ya kwanza yaliyofanyika kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo, London Colney, akiwa na wachezaji wake wote isipokua wale wanaoziwakilisha nchi zao katika fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.
 
Miongoni mwa wachezaji mahiri waliohudhuria mazoezi hayo ni pamoja na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, Aaron Ramsey, Alexandre Lacazette na Shkodran Mustafi, wakianzia mazoezi ya ndani kabla ya kwenda uwanjani.
 
Wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza cha Arsenal walisafiri kwenda Russia na timu zao za Taifa, akiwemo Joel Campbell, ambaye masimu uliopita alikuwa nje ya kikosi akicheza kwa mkopo.
Aidha Kocha huyo amemuita mshambuliaji Lucas Perez alityetumia msimu uliopita kukipiga kwa mkopo Deportivo La Coruna ya Hispania.
 
Mbali na Perez, wachezaji wengine waliokua wakikipiga kwa mkopo msimu uliopita na wanatarajiwa kurejeshwa kundini ni pamoja na Chuba Akpom, Carl Jenkinson na kiungo Jeff Reine-Adelaide.
 
YERRY MINA
Huyu jamaa huko Barcelona ametumiwa Mara chache sana tangu wamnunue toka Palmeiras kwenye dirisha la January, lakini hilo halikumzuia kuonyesha uwezo wake. Na mashabiki wamejionea wenyewe jinsi alivyopambana jana kuhakikisha Colombia inabaki kwenye fainali hizo dhidi ya England na bahati kwenye mikwaju ya penati haikuwa yao
 
Watu wengi hufikiri ya kwamba bahati (nzuri au mbaya) hujijia tu, haibashiriki na ni vigumu kuzuia. Hiyo ni kwa kuwa hawajui maana halisi ya bahati. Ikiwa kama mtu hajui maana halisi ya bahati ni vigumu kuitawala. Waswahili wanasema "mtembea bure si sawa na mkaa bure" pia "bahati ya mbwa ipo kwenye miguu yake"
 
Bahati ni kujitambua dhidi ya uhalisia. Bahati ni kuwa na hisia chanya juu ya tukio au jambo fulani. Mtu mwenye hisia chanya huona kila kitu kinamtumikia (kila kitu kinamsadia kufanikiwa), kwa upande mwingine, mtu mwenye hisia hasi huona kila kitu kinampiga vita; kila kitu huonekana ni kikwazo.
 
Kiasi cha imani (nguvu itokayo ndani) huamua kiwango cha hisia na bahati ya mtu. Mtu anapofanya jambo lolote pasipo imani, kufanya jambo kwa mashaka makubwa, huwa na uwezekano mkubwa kufanya makosa ya kizembe hivyo kujiweka katika nafasi kubwa ya kungeza vikwazo au kukosa kabisa kile alichotaka. Pindi mtu anapojiamini kwa kiasi kikubwa ndipo uwezekano wa bahati (kufanikiwa) unapoongezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…