Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuingia kwenye madeni. Kutaka kujilimbikizia mali kunawafanya watu kukopa kwa pupa na kulipia mambo yasiyo na tija ya kweli kwao. Madeni hayo hupelekea mtu kudhalilika na kufilisiwa baada ya kushindwa kulipa.
 
a9e7bb94d820f35fd18ef1959bfe9bc6.jpg
 
Kuleta tabia hatarishi. Tamaa mbaya hupelekea tabia hatarishi kama kukosa usingizi, kukosa hamu ya kula, hasira n.k. Hali hizo hupelekea kupungua kwa kinga ya mwili na uzito na hatimaye magonjwa
 
Jinsi ya Kukwepa Tamaa Mbaya

1. kukubali mafanikio. Mtu anapaswa kutizama ubora wa mali alizo nazo, ikilinganishwa na awali, bila ya kuangalia nani anamiliki nini. Kuridhia mafanikio ni silaha muhimu sana.
 
Kujitathimini na kuweka malengo. Mtu anapaswa kujiweka mbali na hisia mbaya; hisia za kukosa, na kujiangalia kwa kina mahitaji halisi. Mahitaji halisi huwekwa kulingana na uwezo wa mtu husika.
 
Kukwepa kujithaminisha na mtu.
Mtu asifadhaike kutokana na hatua za mafanikio jamaa zake walizopiga, kwani kila mtu anapata fursa tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti. Pia kamwe mafanikio hayawezi kufanana, kwani mafanikioa ni kama vidole.
 
Kuwasaidia wengine. Kuwawazia na kuwasaidia watu wanaokosa mahitaji ya msingi kama chakula, makazi na mavazi husaidia kupunguza tamaa mbaya kwa kiasi kikubwa, hii ni ngumu sana kwa watu wenye wivu. Ni muhimu kuwasaidia yatima, wajane, wazee wasio na walezi, vilema n.k.
Katika shida na tamaabu zao.
 
Kumwomba Mungu.
Mtu anapaswa kumomba Mungu kadiri ya imani yake, kwani kila mtu anaamini Mungu yupo. Mtu anapaswa kumwomba Mungu ampatie afya, amani, utulivu wa akili na nafsi na mkate wa kila siku; kwani vitu hiyo ni bora kuliko kumiliki mali zenye thamani kubwa kama tani kadhaa za dhahabu.
 
Back
Top Bottom