Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

diversity-tz.jpg
 
Watu wasiokata tamaa; watu wanaoamini kuteleza sio kuanguka; watu wanaoamini kushindwa kufikia malengo kunatoa nafasi ya kujifikiria upya juu ya mwenendo wao, marafiki, mazingira n.k ndio wanaofanikiwa.
 
Katika mataifa makubwa kama Marekani, mataifa yenye fursa nyingi za kufanikiwa; mataifa ambayo yamelegeza sera zao ili kumruhusu mtu afanye anachotaka, takribani 95% ya watu huwa wamefilisika kimaisha wakifika mika 65.
 
Inashangaza! Kuna watu huishi maisha yao ya ujana katika dimbwi la umasikini, wanakuja kupata mafanikio wakifika uzeeni, kwa upande mwingine, kuna watu wanaofurahia maisha yao ya ujana, ili hali wakifika uzeeni huishi maisha duni kabisa.
 
Kuna misemo ya Waswahili kama: mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, (japo kwa sasa, mtaji wa masikini ni akili yake mwenyewe), ndondondo si chururu, kimfaacho mtu chake, heri shika kenda kuliko kumi nenda rudi, n.k
 
Misemo yote kama hiyo inalenga kutoa ujumbe kwamba, nguvu na jitihada za mtu binafsi ndizo zinazomfanya asonge mbele, hasa katika ulimwengu huu wa ushindani. Jitihada za mtu ndio nishati ya kweli inayoweza kumvusha mtu katika kipindi kigumu katika maisha. Haijalishi mtu ana elimu kiasi gani, kama asipodhamiria kufanya kazi, yote ni bure kabisa!
 
Hivyo basi, baada ya mtu kuyumbishwa anapaswa kujitafakari. Kujitafakari ni rahisi ikiwa mtu ataamua kutulia mahali tulivu, huku akitafakari kwa kujiuliza maswali "nilifanya nini? Kwa nini nilifanya hivyo? Kuna nafasi zipi sikizitumia? JE NITAFANYAJE ILI NISONGE MBELE?" n.k
 
Watumiaji wa vyombo vya moto jijini Dar es Salaam watalazimika kutoboka zaidi mifuko kumudu gharama za petroli na dizeli zilizoongezeka mwezi huu.

Ongezeko hilo linafanya watumiaji wa petroli kununua lita moja kwa Sh2,409 tofauti na Sh2,282 mwezi uliopita na Sh2,329 kwa dizeli badala ya Sh2,164.
 
Back
Top Bottom