Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kilwa-3-728.jpg
 
Taarifa ya mwelekeo wa bei kwa mwezi Julai iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha bei ya petroli imeongezeka Sh126 kwa lita, huku dizeli ikiongezeka kwa Sh166.

Kwa takriban miaka miwili ya 2016 na 2017, bei za mafuta hazikupanda kwa kiwango kikubwa kama cha sas
 
Bei elekezi ya Agosti, 2015 ilikuwa Sh2,290 kwa lita ya petroli mkoani Dar es Salaam na dizeli ilikuwa Sh2,026 lakini zilianza kushuka Januari 2016 ambapo petroli ilikuwa Sh1,898 na dizeli Sh1,747.

Akihitimisha mjadala wa bajeti kuu ya Serikali hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema ada, tozo na kodi mbalimbali 19 hutozwa katika kila lita ya mafuta.
 
Taarifa ya Ewura ya jana ilisema mafuta ya taa bei za jumla na rejareja hazijabadilika kwa sababu hakuna shehena mpya ya mafuta hayo iliyopokewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam kwa mwezi Juni.

Ewura ilisema shehena zote za petroli na dizeli (kasoro moja) zilizopokewa katika Bandari ya Dar es Salaam, Juni 2018 zilinunuliwa kwa bei ya soko la dunia ya Mei wakati zilizopokewa Mei zilinunuliwa kwa bei ya soko la dunia ya Machi 2018. “Hivyo, ongezeko la bei za mafuta Julai limetokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia kwa miezi miwili mfululizo ya Aprili na Mei, 2018,” inasema taarifa ya Ewura.
 
Taarifa inasema hakuna shehena ya mafuta iliyopokewa kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi Juni, hivyo bei za petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini zitaendelea kuwa kama zilivyokuwa Juni.

Pia, kutokana na Tanga kuishiwa mafuta ya taa, wamiliki wa vituo vya mafuta katika mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuyanunua Dar es Salaam, hivyo bei za rejareja zitatokana na gharama za mafuta yaliyopokewa katika bandari ya Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.
 
Ewura ilisema Juni 3, kwa mara ya kwanza Bandari ya Mtwara ilipokea meli ya petroli na dizeli kupitia mfumo wa ununuzi wa pamoja (BPS) kwa ajili ya matumizi ya Mkoa wa Mtwara, hivyo bei zimekokotolewa kwa kuzingatia gharama halisi za mafuta hayo yaliyopokewa katika bandari hiyo na gharama ya kuyasafirisha kwenda katika wilaya zote za mkoa huo.
 
Taarifa inasema hakuna shehena ya mafuta iliyopokewa kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi Juni, hivyo bei za petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini zitaendelea kuwa kama zilivyokuwa Juni.

Pia, kutokana na Tanga kuishiwa mafuta ya taa, wamiliki wa vituo vya mafuta katika mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuyanunua Dar es Salaam, hivyo bei za rejareja zitatokana na gharama za mafuta yaliyopokewa katika bandari ya Dar es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.
yaleyale....
 
Watumiaji wa vyombo vya moto jijini Dar es Salaam watalazimika kutoboka zaidi mifuko kumudu gharama za petroli na dizeli zilizoongezeka mwezi huu.

Ongezeko hilo linafanya watumiaji wa petroli kununua lita moja kwa Sh2,409 tofauti na Sh2,282 mwezi uliopita na Sh2,329 kwa dizeli badala ya Sh2,164.
kwisha habari yetu...
 
Back
Top Bottom