Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*Padri alikuwa anafuga kuku.* *Siku moja jogoo akapotea*. *Basi akaamua kutangaza Kanisani.*
*PADRI: Wangapi wana jogoo?* *Wanaume wote wakasimama.*
*PADRI: Sio hivyo jamani! Wangapi* *wameona jogoo? Wanawake wote wakasimama.*
*PADRI: Loh! Hamjanielewa ndugu zanguni!* *Wangapi wamemuona jogoo wangu??* *Masista wote wakasimama.*
*PADRI akapoteza fahamu...!!*
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Vijana tusiharibu lugha bhana
 
[emoji117] Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki[emoji116][emoji818]

Misingi mingine ya ndoa zetu ni migumu sana.
Pata simulizi hii toka Marekani.

Smith na mkewe hawajawahi kuwa na mzozo ndani ya miaka 25 ya ndoa yao. Jambo hili likamfanya jirani yao mmoja kumuuliza Smith amewezaje kuishi na mkewe muda huo wote bila kuzozana! ??

Smith anaeleza:
[emoji117] Tulienda fungate Australia miaka 25 iliyopita, Wakati mke wangu akiwa amempanda farasi, Farasi aliruka na mke wangu akaanguka,
Aliamka akampigapiga farasi kwa upole akasema, "hii ni mara yako ya kwanza"

Baada ya muda ikatokea tena, Alimpigapiga tena na kusema, "hii ni mara yako ya pili"

Farasi alifanya tena mara ya tatu, Mke wangu alitoa silaha na kumuua yule farasi!!!

Nilishitushwa sana na kitendo kile nikamgombeza mke wangu,
- umechanganyikiwa?,
- una matatizo gani?,
- kwa nini umemuua farasi?

Mke wangu aliniangalia, akatabasamu, kisha akasema, "hii ni mara yako ya kwanza"

Tangu siku hiyo nikaushona mdomo wangu,
Hii ndiyo siri ya kuishi miaka yote hii bila kuzozana! [emoji118]
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
kutongoza kijijini kaaaz kwelikweli, nimeenda nikamwona mtoto mzuuuri, nikaanza kumpa mistari, akakaa sawa, akaniomba twende mtoni.. kufika tu akaanza kuvua,[emoji1][emoji1] aaah kuona vile namimi nikaanza kuvua[emoji16][emoji16] tulipomaliza tu kuvua ye akapata samaki wa5 mimi wa2, tukarudi home.. [emoji15][emoji15]umetoa macho ulijua tulivua nn?Huna maana wewe
..
 
Panya mmoja alimeza dhahabu. Mmiliki wa dhahabu ile ikabidi amuite kijana amsaidie kumuua panya yule aliyemeza dhahabu. Baada ya kijana huyu kufika kwa mmiliki wa dhahabu akakuta panya wengi, ila mmoja alikuwa amejitenga pembeni.

Kijana yule akamuua panya yule aliyejitenga, na bahati nzuri ndiye huyohuyo aliyekuwa amemeza dhahabu. Mmiliki wa dhahabu kwa mshangao akamuuliza kijana amewezaje kumjua panya yule kuwa ndiye aliyemeza dhahabu wakati kulikuwa na panya wengi?.

Kijana akajibu, ni kawaida tu kwani hata binadamu akifanikiwa kimaisha basi hujitenga na wengine na kuwaona si hadhi yake.

FUNZO:
Mungu akikuinua kimaisha usiitumie nafasi hiyo kuwaumiza au kujitenga na watu wengine walio na kipato cha chini kwani kujitenga kwako ndio inaweza kuwa chanzo cha kushushwa zaidi.!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…