Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pindi mtu anapofanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kugundulika kwamba anatatizo, taratibu za matibabu hufuata. Ikiwa mgonjwa atakosa ushirikiano kutoka kwa jamaa, rafiki, ndugu n.k zake hukumbwa na hofu, woga, mtizamo hasi n.k. Hivyo hupungua kinga ya mwili na hatimaye kupunguza uwezekano wa kupona kwa haraka.
 
Ikiwa mtu atathibitika ni mgonjwa, jamii inayomzunguka (muuguzaji) inapaswa kufanya yafuatayo ili kufanikisha uponyaji:

1. Kumsikiliza mgonjwa.

Si wagonjwa wote hupenda kuongea, ikiwa yupo, anapaswa kusikilizwa kwa makini na upendo. Ikiwa mgonjwa hapendi kuongea, yapaswa ajengewe mazingira ya upole na utulivu wa akili ili aongee kwa uwazi
 
2. Kuongea juu ya ugonjwa.

Wakati muafaka ukifika, mazungumzo juu ya ugonjwa yanapaswa kufanyika. Mazungungumzo yanaweza kuhusu ukubwa wa ugonjwa katika jamii husika, dalili na matibabu. Mgonjwa anahitaji taarifa sahihi juu ya ugonjwa ili kujiandaa kiakili juu ya hatua zinazofuata. Pindi mgonjwa anapoomba maoni kutoka kwa mlezi, muuguzaji atumie busara ili kutomkwaza mgonjwa.
 
3. Kutodharau.

Ni kawaida kwa wagonjwa kulalamika, hata wengine kumlaumu daktari au Mungu. Katika hali hii, mgonjwa asijibu au kutoa ishara za dharau au kebehi. Muuguzaji ajitahidi kujua sababu za majibu au hisia za mgonjwa, huku akimfariji.
 
Back
Top Bottom