Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbinu II. Kutimiza mahitaji ya wakati husika.
Watu hujipendelea. Watu hupenda mahitaji yao yatimizwe kwanza ndipo ya wengine yafuate. Mshawishi atambue vipaumbele vya msahwishiwa atakavyotekeleza ili maombi yake yatimizwe kwa urahisi.
 
Mshawishi atizame mahitaji, matakwa, vionjo n.k ili aweze kuvuta hisia za mshawishiwa. Mshawishi ajitahidi kutimiza kero au matakwa ya mshawishiwa kwa kadiri ya maadili, hali na uwezo wake kabla ya kutoa ombi lake
 
Mbinu III. Kutoa uthibitisho.
Mshawshi atoe uthibitisho unaoonyesha ya kwamba ombi au lengo lake litatelelezeka bila ya vikwazo vingi. Mshawishi atoe uthibitisho pasipo na shaka ya kwamba atatoa "bidhaa" bora baada ya muda husika; baada ya ombi lake kukubaliwa na kutekelezeka.

Mshindani ashindanishe uthibitisho wake dhidi ya washindani wengine. Mshawishi ahakikishe anayosema au kutoa ni ya kweli na yanawezekana. Msahwishi aonyeshe uhusika au nafasi yake huku akitabasamu ili kukuza imani na urafiki. Pia mshawishi aonyeshe ya kwamba yupo tayari kutoa msaada wa ziada kama ikibidi kufanya hivyo.
 
Mbinu IV. Kuwasiliana kwa ufasaha.
Takribani watu wote wanapenda wakubalike na na kueleweka kadiri wanavyohisi ni sahihi, kwa kadiri ya hisia zao bila kujali jinsi wanavyowasiliana. Mshawishi anapaswa kujiuliza, je niwasilisheje ombi langu bila ya kumkwaza mshawishiwa?
 
Ili kufanya hivyo, mshawishi anapaswa kutumia mbinu za mawasiliano bora zilizoandika katika mada mbili zilizopita. Mshawishi atambue na kukwepa maneno ambayo huathiri hasi utu wa mtu au jamii husika kama yasipotumika kwa kuzingatia mazingiza na aina ya mazungumzo.
 
Back
Top Bottom