Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MANCHESTER United ghafla imeripotiwa kutaka kuwaduwaza wengi kwa kumpeleka ofa ya kumsajili staa wa Barcelona, Ousmane Dembele kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi Ulaya.
Dembele alikumbana na wakati mgumu kwenye msimu wake wa kwanza huko Nou Camp baada ya kuwa na majeruhi ambayo yalimfanya aanzishwe kwenye mechi 14 tu za kikosi hicho kufuatia uhamisho wake wa pesa nyingi kutoka Borussia Dortmund.
 
Barcelona wameripotiwa kuwa na mpango wa kumtoa kwa mkopo staa huyo wa Ufaransa ili kumfanya akawe kwenye ubora wake kabla ya kurudisha kwenye kikosi chao. Kusikia hivyo, kocha wa Man United, Jose Mourinho anataka kuchangamkia fursa. Man United wanataka kumvuta Dembele aje kucheza kwa muda kwenye kikosi chao ili kuongeza nguvu itakayowafanya wapambane na Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.
 
Arsenal na Liverpool nazo zinahitaji huduma ya mchezaji huyo, ambaye kwa sasa yupo kwenye fainali za Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ufaransa. Huko Barcelona, Dembele amefunga mabao manne katika 23 alizocheza kwa msimu wake wa kwanza.
 
SUPASTAA wa zamani wa Croatia, Davor Suker amesema England ina bahati sana kuendelea kuwapo kwenye Kombe la Dunia 2018 hadi sasa.
Suker ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu kabla ya nchi yake ya Croatia haijamenyana na England kwenye nusu fainali ya fainali hizo zinazofanyika Russia kesho Jumatano.
 
Kwenye robo fainali, England waliichapa Sweden 2-0, lakini ilihitaji kushinda kwa mikwaju ya penalti kwenye hatua ya 16 bora walipocheza na Colombia, lakini Suker anaamini taifa hilo lina bahati kuendelea kuwapo kwenye michuano.
Straika Suker, aliyeisaidia Croatia kutinga nusu fainali Kombe la Dunia 1998 alisema: "Nilitazama mechi ya England dhidi ya Colombia uwanjani Spartak huko Moscow walikuwa bahati sana. Colombia walikuwa na nafasi mbili za kufunga kuongoza kwenye mikwaju ya penalti, jamaa wana bahati sana.
 
Suker, ambaye kwa sasa ni rais wa Shirikisho la soka la Croatia ni kinara wa mabao wa muda wote wa taifa hilo baada ya kufunga mara 45 na alishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye fainali za Kombe la Dunia 1998 zilizofanyika Ufaransa.
 
Suker, ambaye kwa sasa ni rais wa Shirikisho la soka la Croatia ni kinara wa mabao wa muda wote wa taifa hilo baada ya kufunga mara 45 na alishinda Kiatu cha Dhahabu kwenye fainali za Kombe la Dunia 1998 zilizofanyika Ufaransa.
 
Kamati ya waamuzi wanaotambulika na Shirikisho la Soka Duniani, imeteua majina waamuzi 12 wa kati, waamuzi wasaidizi 26 na waamuzi 10 wa kutumia teknolojia ya VAR, kwa ajili ya kuchezesha mechi nne za mwisho za Kombe la Dunia, zitakazoanza kesho Jumanne.
 
Kamati hiyo inayoongozwa na Refa wa zamani wa Italia, Peirluigi Collina, imetangaza idadi hiyo mapema leo ambapo mechi ya kesho, iyakayotimua vumbi kuanzia saa tatu usiku, katika dimba la Saint Petersburg inayooingiza mashabiki 64,387, kati ya Ubelgiji na Ufaransa, itachezeshwa na Andres Cunha kutoka Uruguay.
 
Majina ya waamuzi hao watakaochezesha mechi mbili za nusu fainali, mechi ya mshindi wa tatu na mechi ya fainali, itakayopigwa Julai 15, kuanzia saa mbili usiku, kwenye dimba la Luzhniki yenye uwezo wa kuchukua mashabiki 81,000, ni hawa hapa:
 
WAAMUZI WA KATI:

Faghani Alireza (Iran), Diedhiou Malang (Senegal), Geiger Mark (Marekani), Ramos Palazuelos Cesar Arturo (Mexico), Cunha Andres (Uruguay), Pitana Nestor (Argentina), Ricci Sandro (Brazi), Conger Matthew (New Zealand), Cakir Cuneyt (Uturuki), Kuipers Bjorn (Uholanzi), Mazic Milorad (Serbia) na Rocchi Gianluca (Italia).
 
WAAMUZI WA VAR:

Meza ya teknolojia ya video (VAR), itaongozwa na Sampaio Wilton (Brazil), Vigliano Mauro (Argentina), Dankert Bastian (Ujerumani), Dias Soares Artur (Ureno), Gil Pawel (Poland), Irrati Massimiliano (Italia), Makkelie Danny (Uholanzi), Orsato Daniele (Italia) Valeri Paolo (Italia) na Zwayer Felix (Ujerumani).
 
Mwaka 1998, Taifa la Croatia lilifanya kazi kubwa kuwaaminisha wapenzi wa soka kuwa na wao wamo miongoni mwa mataifa yanayopaswa kuogopeka katika ulimwengu wa soka. Walichokifanya pale Ufaransa, hakuna hata mtu aliyetabiri kingeweza kutokea.
 
Back
Top Bottom