Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakiongozwa na mkongwe, Davor Suker, ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Shirikisho la Soka, Croatia ilitinga nusu fainali na kuwaacha watu midomo wazi. Ulimwengu mzima haukuamini ilipoitwanga Ujerumani mabao 3-0 pale Stade Galand.
 
Tangu hapo ilibaki kuhangaika tu. Miaka 20 baadaye, imerudi ikiwa na lengo kuu. Kubeba ndoo na sio kingine. Croatia ina ari, kasi na nguvu ya kufanya hivyo, na msukumo wa kuhakikisha hilo linafanyika limebebwa na Rais wao, Kolinda Grabar-Kitarovic.
 
Utamu utamuni mwanangu

Nyuma ya Kocha wa Croatia, Zlatko Dalic na vijana wake, wakiongozwa na nahodha wao, Luca Modric yupo Rais wa Shirikisho, Suker. Nyuma ya Suker yupo Rais wa nchi, Madam Kolinda Grabar-Kitarovic. Halafu nyuma ya wote hawa kuna vitu viwili, nguvu ya mashabiki na ndoto ya wachezaji.
 
Utamu utamuni mwanangu

Nyuma ya Kocha wa Croatia, Zlatko Dalic na vijana wake, wakiongozwa na nahodha wao, Luca Modric yupo Rais wa Shirikisho, Suker. Nyuma ya Suker yupo Rais wa nchi, Madam Kolinda Grabar-Kitarovic. Halafu nyuma ya wote hawa kuna vitu viwili, nguvu ya mashabiki na ndoto ya wachezaji.
 
Tuanze na hili la Madam Kolinda. Wengi wanajiuliza huyu anaingiaje kwenye mambo ya soka. Ni hivi, shabiki namba moja wa Timu ya Taifa ya Croatia ni Madam Kolinda. Rais huyu ametia fora kule Russia hatari. Tofauti na ilivyo kawaida, Rais Kolinda (50), amekuwa mstari wa mbele kutoa hamasa kwa timu. Kuanzia siku ya kwanza ya fainali hizi, Rais Kolinda alihamishia ofisi yake Russia. Majukumu yake yote ya kitaifa akiyatekelezea katika ubalozi wa Croatia, iliyoko mjini Moscow.
 
Baada ya mechi, Rais Kolinda aliungana na wachezaji katika vyumba vya kubadilishia nguo akiwapa hamasa na hata wakati mwingine alionekana pamoja na wachezaji wake, ufukweni wakila raha.

Kwa staili hii nani ataacha kupambana?

Hii imekuwa siri kubwa nyuma ya moyo wa chuma wa Luca Modric, Ivan Rakitic na wenzao wawapo uwanjani.

Katika mchezo wa juzi Jumamosi wa robo fainali, kati ya Croatia na wenyeji Russia, benchi la ufundi la Croatia lilihitaji ‘sapoti’ ya mwanamama huyu kuvishinda vishindo vya Russia kwenye dimba la Fisht, mjini Sochi.
 
Madam Kolinda alisafiri umbali wa kilomita 1,634, akitumia zaidi ya masaa mawili na dakika 22, kwenda kuhakikisha wanawaua Warusi nyumbani kwao.

Akiwa na jezi ya taifa lake, Rais Kolinda alionekana mara kadhaa pale uwanjani akihaha baada ya Cheryshev kuifungia Russia bao la kuongoza katika dakika ya 31. Dakika nane baadaye, kamera zikammulika akishangalia pamoja na mashabiki wa Croatia waliposawazisha kupitia kwa Andrej Kramaric.
 
....
tapatalk_1531199577283.jpeg
 
SUPASTAA wa zamani wa Croatia, Davor Suker amesema England ina bahati sana kuendelea kuwapo kwenye Kombe la Dunia 2018 hadi sasa.
Suker ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu kabla ya nchi yake ya Croatia haijamenyana na England kwenye nusu fainali ya fainali hizo zinazofanyika Russia kesho Jumatano.
Kweli
 
Katika dakika 30 za nyongeza, Madam Kolinda akiwa amechanganyikiwa, alishuhudiwa akirandaranda karibu na eneo la benchi la ufundi la Croatia, baada ya Russia kupata bao la kusawazisha, kunako dakika ya 115, mfungaji akiwa ni Fernandez. Hatimaye walishinda 4-3 kwa matuta na kusonga mbele.
 
Kama hiyo haitoshi, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo ule, Rais Kolinda aliwafuata wachezaji hadi katika vyumba vya kubadilishia nguo na kuwapongeza akiwapiga kumbatio matata. Asikwambie mtu na baadaye likaangushwa ‘pati’ la kufaa mtu.
 
Back
Top Bottom