NIMEIPENDA HII ANALAYSIS
PASTE AND COPY
Ndugu Wahariri saaam,
Nawaomba katika hili tujiepushe na chembe za siasa ninazoziona nje ya kundi hili. Suala la ununuzi wa ndege yatupasa kuwa na mtazamo mpana kuliko hizi takwimu za kupotosha.
Tujipe muda tusome matumizi halisi. Ndege hii inachoma lita 3.2 kwa sekunde kila inapokuwa hewani sawa na lita 192 hivi kwa dakika au lita 11,520 kwa saa.
Bei ya mafuta ya Jet A1 ni Pound 0.3125 au Sh. 940.315 kwa lita. Kwa Tanzania bei hii iko chini kidogo maana haya mafuta hayalipi kodi yoyote.
Kwa exchange rate ya Paundi 1 = Sh 3,009.01 (source
www.xe.com).
Hii ina maana ndege ikikaa hewani kwa saa moja inatumia Sh 10,832,428.8. Sasa hii dola 13,000 inatoka wapi?
Hii ina maana kwa idadi ya viti ilivyonavyo hii ndege 262 bila kujali madaraja gharama ya mafuta kwa kila kiti kwa kila saa ni Sh 41,345.
Boeing wenyewe wanasema gharama ya kiti ukiweka na handling charges ni dola 23 kwa saa sawa na Sh 52,284.10 (kwa exchange rate ya dola 1 =Sh 2,273.22 source
www.xe.com).
Kwa maana hiyo kwa kasi ya ndege hii ambayo ni kilomita 944 kwa saa Dar -Mwanza inaweza kutumia dakika 50 hivyo itatumia mafuta ya Sh 9,027,024 kwa dakika 50.
Bei ya chini kwa hapa kwetu ni Sh 160,000 safari ya Dar Mwanza. Hivyo ikipata wastani wa wateja 100 tu kwenda, itakusanya Sh mil 16 na ikipata pia 100 kurudi inakusanya nyingine 16 mil. Na kuwa Sh mil. 32.
Ikijaza kwenda na kurudi Dar Mwanza itakusanya Sh 83,840,000 ndani ya muda wa saa 2; yaani kwenda Mwanza na kurudi Dar.
Umbali kati ya Dar -Mwanza kwa ndege ni maili 530 au kilomita 853.
Hapa kwetu bei ya mafuta ya Jet A1 iko chini zaidi maana mafuta ya ndege hayalipi kodi yoyote.
Mashirika ya Ndege ya Emirates na Ethiopia Airline yanapata faida ya kati ya asilimia 25 na 35 juu ya gharama za uendeshaji kwa mwaka.
Biashara ya ndege ina faida kubwa ila tatizo hapa kwetu lilitokana na wizi wa watumishi. Tiketi watu wazima walikuwa wanakatiwa za watoto lakini wakati wa kushuka inaonekana kila mtoto kanywa bia 5, bei zinawekwa za mkomoeni...
Nihitimishe kwa angalizo: Kwa muda mrefu Afrika imetawaliwa na Wazungu kwa njia ya takwimu na taarifa feki.
Wanapenda kutukatisha tamaa katika kila tufanyalo waendelee kututawala.
Zitto amegusia utalii, bila ndege imara na za kisasa mlima wetu wa Kilimanjaro utaendelea kuhesabika uko Kenya, itatangazwa Maasai Mara kama vile inaizidi Serengeti na Ngorongoro.
Ethiopia leo imeshika nafasi ya kwanza duniani katika kuuza maua Ulaya kwa sababu wanamiliki ndege.
Samaki wetu tunaweza kuwauza kwa bei nzuri katika supermarket kaka Asida, Sainsbury's, Tesco na mengine huko Ulaya kwa kuwa na National Carrier.
Lakini si hilo tu, Wakurya wanapanda malori ya mizigo wanalipishwa Sh 50,000 Dar Mwanza, wanalala njiani siku 3; wanakula, wanakunywa na hadi wanafika Mwanza ukiacha muda wa siku 3 waliopiteza wanatumia hadi 100,000 njiani!!!!
Time is money. Saa 1 unatoka Dar hadi Mwanza unafanya kazi na kurejea. Naamini Watanzania tunahitaji ndege zaidi kuliko mabasi na hii itatusaidia kuwakwepa matrafiki wanaopiga faini ya Sh 30,000 hata kama uko speed 51.
Pia, ndege hazina ajali za kijinga. Katika hili Rais Magufuli apongezwe, asibezwe hata chembe, ila wanaobeza kazi hii waelimishwe wasifungwe maana wako huru kutoa mawazo yao na tuwe tayari kusikia hata tusiyoyapenda.
Nawasilisha.
Balile, D.