Methali zimekwisha muda wake wa matumizi.
Mfano:
1. Mwenzako akinyolewa tia maji.
-Siku hizi tunanyoa kwa mashine. Ukitia maji zinateleza hazinyoleki.
2. Barua ni nusu ya kuonana.
-Siku hizi watu wanaonana kwa WhatsApp. Mkingojea barua mtakufa bila kuonana.
3. Akili ni nywele.
-Vipi kuhusu Mawigi?
4. Mchagua jembe si mkulima.
-Siku hizi tunatumia zaidi matrekta ya kukodi.
5. Alalae usimuamshe akiamka utalala wewe.
-Siku hizi unaweka alarm mwenyewe unaamka hausubiri kuamshwa na mtu.
6. Polepole ndio mwendo.
-Siku hizi kuna mwendo kasi ukienda polepole utabaki.
Hatupendi mambo ya kizamani...