Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Real Madrid imekubali Cristiano Ronaldo ajiunge na Juventus, lakini sasa wanataka kujenga timu mpya hiyo ni wazi sasa watalazimika kusajili Galacticos wawili ili kulinda heshima ya klabu hiyo.

Urafiki wa Florentino Perez na mshambuliaji huyo Mreno umefika mwisho, hata hivyo rais huyo atalazimika kutafuta mrithi wa nyota huyo wa zamani wa Manchester United haraka.
 
Kila mmoja kuanzia mashabiki hadi viongozi wote wanasubiri kusikia kutoka kwa Perez atamsajili mshambuliaji gani mpya wa kuziba pengo la Ronaldo.

Real inaweza kufanikiwa bila ya Ronaldo, lakini ni wazi wanatakiwa kusajili mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kiwango kile alichokuwa akionyesha nyota huyo mwenye miaka 33.
 
Real Madrid ina fedha, lakini ni wachezaji wa aina gani wanataka kumsajili katika mazingira ya sasa na ugumu wake upo wapi.

Neymar ni chaguo la kwanza, lakini nyota huyo wa Brazili kuhamia Madrid inatakiwa nyota huyo wa zamani wa Barcelona anatakiwa kurudia kile alichokifanya Ronaldo kwa kuvunja ukaribu wake na Nasser Al-Khelaifi ili aweze kuachwa na mmiliki huyo wa Paris Saint-Germain.
 
Mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe ni chaguo lingine, itakuwa vigumu kwao kumnasa si kwa sababu ya fedha bali ni malengo binafsi ya chipukizi huyo.

Mchezaji anayeweza kupatikana kwa haraka na wepesi ni Eden Hazard, nyota huyo wa Ubelgiji anaweza kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya iwapo Chelsea watakuwa tayari kupokea dau la euro 100 milioni.
 
PAUL Pogba alikuwa na jambo moja baada ya timu yake ya Ufaransa kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2018 kwa kuifunga Ubelgiji, kuingia kwenye ukurasa wake wa Twitter na kutuma ujumbe maalumu kwa wale watoto 12 wa timu ya soka waliokuwa wamenaswa kwa pango huko Thailand.
 
Watoto hao ambao waliokolewa kutoka kwenye pango hilo wakiwa na afya njema kabisa, waliripotiwa kupata mwaliko wa kwenda kwenye Kombe la Dunia 2018 kuhudhuria moja ya mechi hizo, ambazo kwa sasa zimebaki mechi mbili tu, kuwania mshindi wa tatu na ile ya fainali itakayopigwa Jumapili
 
Wakati Pogba afanya hilo, hakuwa na ufahamu kama klabu yake ya Manchester United inatoa mwaliko kwa watoto hao 12 kwenda kutembelea Old Trafford. Tukio la ukoaji wa watoto hao lilikamilika juzi Jumanne baada ya siku tatu za waokoaji kupambana kuwatoa kwenye pango watoto hao walipokuwa wamebanwa baada ya mvua kubwa kunyesha wakati wakiwa chini ya pango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…