Hilo tukio silijui labda kama ni mambo ya utawala tofauti na idara yangu, nachoweza kusema ni kwamba tulipomaliza Ligi tulivunja kambi wanafunzi wakaendelea na mitihani" amesema Budodi.
Hata hivyo Mkurugenzi wa kituo hicho, James Bwire alipotafutwa amesema yeye hajui lolote licha ya kupigiwa simu kumuuliza suala hilo na kusema kuwa atafutwe baadaye.
"Mimi hilo suala hilo silijui, napokea simu tofauti naulizwa, lakini sijui kabisa lakufanya nitafute tena baadaye nitakuwa nimetulia," amesema Bwire.