myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Tafiti zimeshaonyesha kuwa usomaji wa vitabu umeporomoka sana kwa Tanzania. Riwaya pendwa za kipelelezi za akina Musiba, Katalambula, Mtobwa na waandishi wengineo zilivutia wasomaji wengi katika miaka ya 80 na kipindi hicho kinatambuliwa leo kuwa kipindi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili. Leo hii mpaka ubahatishe kitabu chako kiingizwe katika mitaala ya shule. Watu hawaoni sababu ya kuingia gharama kuchapisha kitabu wakati mauzo yake ni hasara tupu.
Kuna makala mengi ya kitaaluma kuhusu jambo hili na kwa nini leo vitabu vingi vinatoka Kenya.