Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku chache kupita baada ya Cristiano Ronaldo kusajiliwa kwa dau la Pauni 100 milioni, nyota huyo ameonekana akiwa na familia yake, huku mwanaye akiwa ametinga jezi ya Juventus.
Nyota huyo alitambulishwa rasmi juzi Jumatatu kuwa mchezaji wa Juventus kwa mkataba wa miaka minne.
 
Hata hivyo, Juventus na Real Madrid zinatarajiwa kukutana nchini Marekani kwenye mchezo wa kirafiki Agosti 4, huku ikielezwa kuwa Cristiano Ronaldo hatacheza.
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania inatarajiwa kutangazwa rasmi Ijumaa wiki hii.
Nyota ahuyo alifunga mabao manne kwenye Kombe la Dunia lililomalizika Jumapili wiki iliyopita kwa Ufaransa kunyakua taji la Kombe la Dunia mwka 2018.
 
Klabu ya Liverpool, imetakiwa kukamilisha haraka uhamisho wa kiungo mshambuliaji Nabil Fekir, vinginevyo inaweza kumkosa.
Klabu ya Lyon imeipa Liverpool muda wa mwisho kukamilisha uhamisho na ikishindwa itamuondoa sokoni mchezaji huyo na kumjumuisha katika kikosi kinachojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Ufaransa.
Fekir aliyecheza Lyon mechi 115 na kufunga mabao 45, alikaribia kutua Liverpool katika usajili uliopita, lakini uhamisho wake ulikwama dakika za mwisho kutokana na ukubwa wa ada Pauni 53 milioni.
 
Rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas, alisema Liverpool isipokamilisha uhamisho huo mapema, itamlazimisha mchezaji huyo kujiunga na wenzake wanaoanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi.
Fekir aliyeng’ara katika fainali za Kombe la Dunia licha ya kucheza akitokea benchi, alisisitiza anataka kutua Makao Makuu Anfield alikoahidiwa mkataba wa miaka mitano na mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki.
 
Klabu ya Barcelona ya Hispania, imejitosa kuwania saini ya kiungo mahiri wa Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin, Miralem Pjanic raia wa Bosnia na Herzegovina.
Barcelona imeibua vita ya aina yake katika kuwania saini ya mchezaji huyo ambaye alianza mazungumzo na mabingwa wa Ligi Kuu England, Man City.
Juventus imeridhia kumuuza mchezaji huyo muda mfupi baada ya kutoa Pauni 105 milioni kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.
 
Juventus inataka kuwauza baadhi ya wachezaji ili kukamilisha fedha za kumnunua Ronaldo kwa kuhofia kanuni za fedha za usajili za Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa),” ilisema taarifa ya klabu.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola, ameweka bayana nia ya kumsajili Pjanic ambaye ni kiungo bora Juventus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…