Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20180720-WA0020.jpg
 
*Tumsifu Yesu Kristu*
*Ikiwa Leo ni siku ya Ijumaa ni siku ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.* *Upendo wa Kristu kwetu hauna mipaka wala mwisho, Upendo wa Mwanadamu ni wa masharti na una mwisho wake.*
*Kristu alitupenda upeo, hata akaitoa nafsi yake kufa Msalabani kwa ajili yetu sisi.*
*Leo hii tumekuwa ni watu wa kulipishana visasi, Mmoja akimwaga ugali mwingine anamwaga mboga.* *Maisha yetu ya leo yamejaa Usaliti mtupu, Uwongo umetawala vinywa vyetu ,kila kuchao siku hizi kilichobaki ni kuumizana, kunyoosheana vidole na kulaumiana.*
*Hayo yote yanaujeruhi Moyo Mtakatifu wa Yesu. Ishi na kila mtu vizuri, wapende watu wote, ishi kwa roho ya Msamaha, wasamehe bure wale watu wote waliokukosea , utawabeba mpaka lini. Utaumia mpaka lini!*
*Ee Yesu tunakuomba Damu na Maji yako visipotee bure bali vitupatie uzima wa Milele.*
*Moyo Mtakatifu wa Yesu Utuhurumie.*
*Moyo Mtakatifu wa Yesu ufalme wako ufike*
 
Back
Top Bottom