Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

viagra au vega,ni dawa inayotumika sana miongoni mwa wanaume kwa lengo la kuongeza uwezo wao wa kufanya mapenzi ( sex),dawa hizi mara nyingi zinatumiwa na watu wenye matatizo katika mfumo wa uzazi yaani wasioweza kusimamisha vizuri kiungo cha uzazi lakini pia,imekua ikitumikahata kwa watu wasio kua na tatizo hilo ila anaitumia kwaajili yakumkomoa mwanamke flani na wengine hupenda kuiga vile wanavyofanya waigiza sinema za ngono (porn graph). bila kutambua madhara yake makubwa watu wanajiingiza kuzimeza dawa hizi,kwaleo napenda kukufahamisha jinsi inavyofanya kazi na madhara yake.
 
JINSI INAVYOFANYA KAZI:
Viagra,haimfanyi mtu kupata ashki ya kufanya ngono bali yenyewe hufanya kazi endapo tu mtu atakua amepata ashki ya kufanya ngono. ili upate kuelewa jinsi inavyofanya kazi nibora kuelewa jinsi mwanaume anavyoweza kusimamisha uume. pindi mwanaume anapopata ashki ya kufanya mapenzi,mishipa ya mfumo wa fahamu ( nervours system) ilioko katika misuli ya uume hutoa kemiko zinazoitwa Nitric oxide (NO), ambayo huamrisha viamshi ( enzymes) kuzalisha kemiko zingine tena zinazoitwa messenger Cyclic guanosine monophosphate ( cGMP ).
 
cGMP huifanya misuli laini ya uume kujiachia na kutanuka ambapo matokeo yake huiruhusu damu kuingia na kujaa vizuri katika mishipa midogomidogo ( blood cappilaries) ilioko katika uume, hapo ndipo uume unaposimamavizuri sasa. hivyo basi Viagra hufanya kazi ya kusawazisha kiwango cha hii kemikali inayoitwa Cyclic guanosine Monophosphate ( cGMP )
 
).madhara ya Viagra ;kwa mara ya kwanza dawa hii ilitumika kutibu tatizo la pressurelakini ilionesha maajabu sana pale ilipo onekana kuwafanya wagonjwa kua na nguvu nyingi sana za kusimamisha maumbileyao ya uzazi, baada ya hapo zikazuiwa kutumika mahospitalini lakini baadae zikafanyiwa uchunguzi na zikarudishwa tena rasmi kwaajili ya watu wenye matatizo ya kusimamisha, ilikua ikitumika kwa watu hasa waliokosa nguvu za kiume kwasababuza kisaikolojia hivyo basi chini ya usimamizi wa dactari walikuawanapewa dawa hizi huku wakipewa ushauri nasaha ili wajiamini kua wanauwezo wa kufanya vizuri tendo hilo baada ya muda flani mgonjwa hurudi katika hali yake ya kawaida na kuacha kuzitumia dawa hizi lakini kwa sasa watu wengi wanatumia hata kama anatatizo la mfumo wa uzazi bado atalazimishia tu kuzitumia matokeo yake ni kama ifuatavyo;
 
Mtu anaetumia viagra bila ushauri wa dactari huku akiwa na matatizo mengine ya kiafya kama pressure yuko hatarini kupoteza ihai wake.
 
Kadri mtu anavyotumia Viagra ndivyo tatizo linavyozidi kua baya zaidi, kwasababu viagra inamfanya asimamishe kwa muda mfupi hivyo akitaka kufanya mapenzi siku ingine lazima azimeze tena dawa hizi hali hii ya kuzimeza kila wakati inamfanya kua torelance ( tegemezi hali ya kumfanya azidi kuongeza dozi yake ili apate nguvu zinazomtosheleza ) mwishowa siku dawa hizi hutengeneza sumu mwilini na kuua kabisa nguvu za kiume.
 
Mtu anaetumia Viagra yuko hatarini kupata ukiziwi,

~ mtu anaetumia viagra ,yuko hatarini kupoteza uwezo wa kuona hii ni kutokana kwamba dawa hizi hua baadhi ya viachocheo vinavyofanya kzai ya kusafirisha mwanga na picha kuelekea katika mfumi wa fahamu kuharibiwa na dawa.
 
hivi.kulikoni kutumia dawa hizi ni bora ukatafuta dawa za mitishamba,mbona kunadawa za mitishamba nimeshuhudia zikifanya kazi kwanini basi watu bado wanakimbilia chemotherapy ambazo zinaongeza magonjwa miilini mwetu. Napenda kukushauri kueoukana na kukimbilia kutumia dawa hozi Viagra ni hatari sana.
 
FAIDA YA JUISI YA UKWAJU

Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.
 
NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.
Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarketsAndaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.
 
FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.
Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumboHuulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooniHusaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwaHusaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)Husaidia kurahisisha choo (laxative)Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyoHusaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidondaHusaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
 
Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!

Unatakiwa ujaribu kuweka
ukwaju karibu katika kila mlo
wako kwa kila siku kwasababu
ukwaju una faida nyingi kiafya
ambazo hakika zitakufanya uwe
na afya njema au kukuimarisha
afya yako kiujumla
 
Watu waishio bara la Asia,
Carribian na America ya kusini
wanajua kuwa kula ukwaju
maana yake ni Afya Njema.

Ukwaju unaoliwaa katika maeneo
haya maeneo hayo una faida
nyingi kwa watu wanaoula.
 
Kwa hiyo siku nyingine unapoenda
kufanya manunuzi ya vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia
ambalo limefungwa na kasha
gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani
yake kuna mbegu nyeusi.
 
Vifundo
hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju. Ukwaju
una ladha faluni ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri
unavyozidi kukomaa unakuwa na
ladha tamu. Ingawa ukwaju
unakuwa na utamu kadiri
unavyokuwa na kukomaa,
kiujumla ukwaju ni mchachu.
 
Katika nchi kama Jamaica, Mexico,
Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na
kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwajua au
bidhaa zitokanazo na ukwaju
kuna faida sana. Ukwaju umejaa
Vitamini, fiber, potassium,
magnesium na virutubisho
vingine muhimu kwa afya njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…