Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

76aaf79b-a98a-470b-9957-0f5067f38de3.jpg
 
Miguu ni sehemu ya mwili inayotumika sana inatumika katika kutembea na kufanya shughuli zako za kila siku. Hii inamaanisha miguu inabidi iangaliwe zaidi na ipewe care ya hali ya juu ili kuifanya iendelee kukubeba na kufanya shughuli zako za kila siku. Kujali na kuiangalia miguu yako itakusaidia sana kuepukana matatizo ya ngozi za miguu kama Athlete’s foot au aina nyingine ya fangasi . Wakati wote miguu yako inatakiwa iwe katika hali nzuri na ya kupendeza.
 
Katika kutimiza majukumu yako ya kila siku tunatembea sana toka sehemu moja kwenda nyingine, miguu inakuwa imepitia kwenye vumbi na uchafu kibao pale siku inapoisha. Fanya zoezi la kuiosha miguu yako ni sehemu ya utaratibu wako wa kila siku kabla hujalala hata kama hutaoga usiku huo . Isafishe vizuri kwa sabuni huku ukizingatia zaidi sehemu za katikati ya vidole vyako. Futa miguu yako kwa taulo au kitambaa kisafi na kikavu kwa umakini zaidi ili unyevu wote uishe, usilale na miguu iliyo na unyevu ni mwanzo wa kuzalisha vijidudu vya kuleta harufu mbaya.
 
Sio lazima kupaka rangi kucha kila unapofanya pedicure kama si mpenzi wa kupaka rangi, ila pedicures zinasaidia sana kufanya nyayo na vidole vyako viwe laini na nyororo huku ukiondokana na ngozi ngumu/magaga. Si lazima ifanyike saluni na upoteze hela, inaweza ikafanyika nyumbani kwako kwa kufuata hatua zifuatazo
 
Loweka miguu yako kwa dakika 5 – 10 katika beseni kubwa lenye maji uvuguvugu. Unaweza kuongeza matone ya mafuta kama olive oil au hata lotion uitumiayo mwilini ili kuongeza moisture na kufanya miguu ilainike zaidi. Unaweza ukailoweka kwa muda wowote uupendao kama utapenda zaidi kurelax na kuifanya ngozi yako ilainike zaidi.
 
Sugua miguu yako kwa kutumia scrub ili kuondoa layer ngumu na iliyokufa ili ubaki na layer laini. Kusugua/exfoliate ngozi ngumu ya kisigino sugua kwa kutumia brush au jiwe maalumu la kusugulia hakikisha unasugua kwa utaratibu kiasi na si kwa nguvu sana ili kukupunguzia maumivu ndiyo ni ngozi ngumu lakini kama layer ngumu ikitoka inabaki delicate skin ambayo ni laini na nyororo!
 
Kata kucha zako katika shape uipendayo ila hakikisha si katika shape ya mduara ili kupunguza tatizo la kucha kuotea kwa ndani (ingrown toenails). Kama unapenda shape ya mduara waweza kuzikata katika shape ya kawaida na ukazipiga msasa/file kuzipa umbo ulipendalo. Hakikisha kucha unazikata katika urefu wa kawaida zisiwe fupi sana.
 
Kumbuka ngozi inayoizunguka kucha zako/cuticles waweza kupaka mafuta kiasi au lotion uipendayo ili kuzilainisha na zirudishe nyuma kiasi kwa kutumia kijiti maalumu cha kufanyia hivyo. Angalizo usirudishe sana ngozi hiyo nyuma unaweza ukaijeruhi na ni rahisi kupata maambukizo ya fangasi kama hilo likitokea. Kuna watu hawapendi kusogeza cuticles zao ni uamuzi sahihi tu.
 
Back
Top Bottom