Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JINSI YA KUKUZA NYWELE ZENYE DAWA.
1.Hakikisha unachagua dawa ya nywele inayoendana na nywele zako..mimi natumia movit..kwakuwa nywele zangu ni nywepesi sana nawekaga chini tu
2.lazima upange muda wa kuweka nywele dawa...Mimi huwa naweka baada ya miezi mitatu
3.suka mitindo rafiki na nywele zako usipende kusuka tu kila mtindo chagua mitindo ambayo haitakata nywele
 
4.hakikisha unaosha nywele zako Mara kwa Mara...angalau Mara 3 kwa mwezi au 2
5.Tumia mafuta rafiki na nywele zako..mafuta yenye uwezo wa kutunza unywevu na kuzuia nywele kukatika Mimi natumia beautifully hair oil..
6.punguza matumizi ya moto kwenye nywele..mfano.kupasi nywele..hii hufanya nywele kutokuwa na nguvu usitumie Mara kwa mara
7.Uwe ukilala na plastic (satin)zile kofia za mfuko..zinasaidia nywele kufyonza mafuta na kumaintain Ph
 
Wengi wetu huwa tuna dhani kuweka dawa na kufanyia steaming ndio kutakuza na kufanya nywele zetu kuwa na afya, hivyo utakuta mtu ana weka dawa kila baada ya mwezi na kufanyia steaming kila baada ya week mbili. Hii ndio husababisha nywele kunyonyoka na kutokua na afya.
 
Dawa si nzuri sana kwa nywele zako hivyo una shauriwa kuweka dawa mara mbili au tatu kwa mwaka. Hii ina maana uweke dawa kila baada ya miezi sita hadi minne. Lakini swali linakuja je katika kipindi hiko chote ambacho nywele zina oteana na kukua uta fanyaje hili zisikatike? hizi ndizo tips muhimu za nini ufanye
 
1) Deep Condition – fanyia deep condition mara kwa mara hii itasaidia kurainisha nywele zako na kuipa nywele afya, wakati una fanyia deep condition ni vizuri ukaosha nywele na maji ya baridi na pia usikae kwenye moto, paka condition yako funga mfuko wa plastic na taulo juu kaa nalo kwa nusu saa osha.
 
2)paka mafuta ya nywele kila siku – hii ni muhimu mno kwa nywele zako uli kuzipa nywele unyevu na kurainisha ili kuzuia ukatikaji wa nywele ni muhimu uwe una paka mafuta mara kwa mara, na mafuta mazuri kwa ajili ya nywele ni mafuta ya kumiminika na si mafuta ya mgando. Eg olive oil ya maji au mafuta ya nazi ya maji.
 
4) Suka misuko ambayo haikati nywele – ipo mingi sana una weza ku google “protective hair styles” ukaipata lakini pia nywele za kurudi nyuma “twende kilioni” husaidia mno ndio maana utakuta wanafunzi wengi wana nywele ndefu zilizo na afya.
 
5)Punguza kukaa/kutumia vitu vya moto – kutumia pasi au dryer kukaushia au kunyooshea nywele mara kwa mara kuna athiri nywele, nywele hupoteza ubora wake kutokana na moto. Hii huathiri hata zile nywele zinazo ota. Kama una osha nywele mara kwa mara ni vyema ukaziacha zikauke zenyewe na upepo.
 
Back
Top Bottom