Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mnakoelekea sio wahusika omben uzi ufutwe

Kuna mwanaume mashine na mwanaume suruali

Naongelea hapa ,pengine mmmh so sad kwa hizo screenshot
Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na kamwe mwanaume hagombani na wanawake.
Sasa tangu jana anachambwa yeye tu na yeye anajibizana na wanawake kweli?
Ila acha sisi tule ubuyu tutafanyaje sasa
 
EDEN Hazard kama kipusa anasakwa. Kitu kizuri zaidi, hata yeye mwenyewe analipenda hilo.

Staa huyo fundi wa mpira ameripotiwa kupewa ofa ya mkataba wa Pauni 13 milioni kwa mwaka ili akajiunge na Real Madrid kwa uhamisho wa Pauni 170 milioni, jambo litakalomfanya kuwa mchezaji namba mbili ghali zaidi duniani baada ya Neymar.
 
Real Madrid wanataka kutumia fursa hiyo ya kumsajili Hazard kwanza kwa sababu Chelsea imebadili kocha, wamemwondoa Antonio Conte na kumleta Maurizio Sarri, pili wanahitaji mchezaji mwenye uwezo wa kwenda kufuta machungu ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo, aliyetimkia Juventus dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.
 
Hazard mwenyewe anaonekana kukaribisha dili hilo la kutimkia Bernabeu na hakika ni uhamisho ambao una nafasi kubwa ya kutokea hasa baada ya wakali wengine ambao Los Blancos ililenga kuwasajili, Neymar na Kylian Mbappe wote kuonekana hawapo tayari kuondoka Paris Saint-Germain.
 
Hata hivyo, kama ilivyo kwa Real Madrid wanaohangika kutafuta mrithi wa Ronaldo, staa Hazard naye akiondoka Stamford Bridge ataacha pengo litakalohitaji kutafutwa mtu wa kuja kuliziba.
 
Hii hapa orodha ya wachezaji ambao hakika wataweza kuhamia Chelsea na kwenda kuwaondolea machungu ya kumpoteza Hazard kama staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ataamua kwenda zake Bernabeu kutafuta changamoto mpya.
 
Lorenzo

Insigne, Napoli

Ni mshambuliaji matata kabisa na Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri anamfahamu vyema kwa sababu alifanya naye kazi huko Napoli. Insigne linaweza kuwa chaguo mwafaka katika kurithi buti za Hazard huko Stamford Bridge hasa ukizingatia hata kocha wa kikosi hicho kwa sasa anafahamu makali na udhaifu wa mchezaji huyo, hivyo itakuwa vyema na atakwenda kuungana na staa mwenzake mwingine wa zamani wa Napoli, Jorginho, ambaye tayari ameshanaswa na wakali hao wa Ligi Kuu England.
 
Dries Mertens,

Napoli

Ni mchezaji mwingine ambaye alikuwa kwenye kiwango bora kweli kweli chini ya Sarri huko Napoli. Pengine, Mertens anaweza kuwa mshambuliaji wa aina tofauti kabisa na kumlinganisha na staa mwenzake wa Ubelgiji, Hazard kutokana na staili yao ya kiuchezaji, lakini ni chaguo ambalo halitakuwa baya sana kwa Chelsea kama wataamua kulifanya kutokana na kuondokewa na mchezaji wao huyo makini.
 
Kocha Sarri anamfahamu vyema Mertens na kwa siku za karibuni amekuwa kwenye kiwango chake bora kabisa kilichokuwa kikifanya Napoli kuwa timu ya kuogopwa msimu uliopita.
 
Back
Top Bottom