Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nabil Fekir, Lyon

Ndiyo hivyo, Fekir haendi tena Liverpool. Kwa maana hiyo, huduma yake inapatikana tu ni suala la Chelsea kuchangamkia tu fursa ya kwenda kuinasa huduma yake. Liverpool walishindwa kukamilisha dili la kumsajili supastaa huyo wa kimataifa wa Ufaransa ikiwa ilishamfanyia hadi vipimo vya afya na kuachana naye kama ilivyofanya kwa Loic Remy mwaka 2014. Kutokana na hilo, Chelsea wanaweza kufanya kweli na kumsajili Fekir kumleta kwenye kikosi chao kama Hazard ataondoka kwa sababu staili ya kiuchezaji ya wawili hao inaonekana kufanana. Ni chaguo jingine bora kwenye mpango wa kunasa huduma ya staa huyo kuja kuziba pengo la Hazard kama ataondoka.
 
Wilfried Zaha,

Crystal Palace

Ni chaguo ambalo litakuwa na maswali mengi, lakini hakuna ubishi Zaha mipango yake kwa sasa ni kwenda kwenye timu itakayompa nafasi ya kukua zaidi ili kupandisha soka lake kutoka pale alipo kwa sasa huko Crystal Palace. Kasi na nguvu ndicho kitu kinachomfanya Zaha kufanana kiuchezaji na Hazard, lakini shida ya Zaha ni moja tu, amekosa usahihi wa mipira yake ya uwanjani, tofauti na Hazard, ambaye amekuwa na uamuzi mkubwa anapokuwa na mipira kwenye miguu yake. Zaha ameshawahi kucheza kwenye timu yenye presha kubwa kama Manchester United, lakini timu hizo mbili ni tofauti kabisa, pengine akienda zake Chelsea atakwenda kukutana na timu isiyokuwa na presha kubwa sana na anaweza kufanya vizuri.
 
Ivan Perisic,

Inter Milan

Yule staa aliyewafanya vibaya England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia walipomenyana na Croatia, Ivan Perisic anafahamika vyema na Sarri baada ya huduma yake anayotoa huko Inter Milan. Kwenye dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi, Perisic alikaribia kabisa kujiunga na Manchester United, hivyo suala la kuja kwenye Ligi Kuu England si jambo gumu kufanywa kwa winga huyo aliyekamilika katika kila idara. Sawa, hana ule ujuzi mkubwa wa kuufanya mpira ufanye anachokitaka kama alivyo Hazard, lakini Perisic ni mchezaji mzuri ambaye ukiwa naye kwenye timu lazima huduma yake itakuwa inakuvutia. Kwenye dirisha hili la usajili, kocha wa Man United, Jose Mourinho alionekana kumtajataja, haifahamiki kama atajaribu tena kutaka kumsajili.
 
Julian

Draxler, PSG

Mengi aliambiwa supastaa wa Kijerumani, Julian Draxler kwamba atakwenda kukutana na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza katika kikosi cha PSG na hakika hilo ndilo lililotokea. Sawa, alibahatika kuwapo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia shukrani kwa kocha Joachim Low, lakini ukweli unabaki palepale, Draxler anahitaji kwenda kucheza timu ambayo itampa nafasi ya kucheza kila wiki. Wakati Chelsea wakielekea kumpoteza supastaa wake Hazard anayewindwa kwa nguvu zote huko Real Madrid, wababe hao wa Stamford Bridge wanaweza kuhamishia nguvu zao kwenye usajili wa staa huyo wa Kijerumani na hakika Draxler mwenyewe anapaswa kuchangamkia nafasi hiyo kama italetwa ofa mezani kuhitaji saini yake.
 
Thorgan Hazard

Ni hivyo, kama unashindwa kuwa na Hazard mmoja, kwanini usiwe na Hazard mwingine? Thorgan naye aliwahi kuwa Chelsea, lakini aliondoka kwenda Borussia Moenchengladbach kwenye Bundesliga mwaka 2015. Kwa sasa kiwango cha Thorgan kinaonekana kukuwa kwa kiasi kikubwa sana na huko kwenye Bundesliga amekuwa akivaa jezi namba 10 kama alivyo kaka yake huko Stamford Bridge. Uchezaji wa wawili hao unafanana, hivyo Chelsea wanaweza tu kumbadili Hazard kwa kumvuta mdogo wake kwenye kikosi chao na mambo yatakuwa matamu tu.
 
Back
Top Bottom