Ivan Perisic,
Inter Milan
Yule staa aliyewafanya vibaya England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia walipomenyana na Croatia, Ivan Perisic anafahamika vyema na Sarri baada ya huduma yake anayotoa huko Inter Milan. Kwenye dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi, Perisic alikaribia kabisa kujiunga na Manchester United, hivyo suala la kuja kwenye Ligi Kuu England si jambo gumu kufanywa kwa winga huyo aliyekamilika katika kila idara. Sawa, hana ule ujuzi mkubwa wa kuufanya mpira ufanye anachokitaka kama alivyo Hazard, lakini Perisic ni mchezaji mzuri ambaye ukiwa naye kwenye timu lazima huduma yake itakuwa inakuvutia. Kwenye dirisha hili la usajili, kocha wa Man United, Jose Mourinho alionekana kumtajataja, haifahamiki kama atajaribu tena kutaka kumsajili.