Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hahahahahaa[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kucha kama kisu cha kukeketea dah noma [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jana saa nane mchana, tukio la ajabu imetokea shule ya msingi Emaco mjini Geita. Mwanafunzi mmoja pichani (Traki nyeusi) amewawekea wenzake sumu kwenye chakula. Mtoto wa darasa la nne (Traki bluu) alishuhudia tukio na kutoa taarifa kwa mwalimu. Baada ya mahojiano mafupi na huyo dogo aliyeweka sumu akasema kuwa kapewa na dada mmoja ili awaue wanafunzi wenzake wanaomsumbua shuleni. Mungu amenusuru kwa kuwa chakula kilikuwa hakijafika kwa walengwa, mtoto amefukuzwa shule na hatua zingine zinafuata.
 
Sio kila EX Wako anayeomba mrudiane anamaanisha, wengine huomba kurudi Ili wakutesti tu jinsi ulivyo dhahifu, Jinsi usivyo na msimamo na jinsi ulivyo CHEAP na huna misimamo wala future. Mtu mmeachana miezi 6 iliyopita, leo anakutesti mrudiane, na wewe ulivyo mvivu wa kifikiri, upo upo tu, alafu unajikuta tena ukimpa fursa nyengine ya kuendelea kukuchezea. Ina maana miezi yote hiyo ulikuwa umeganda unasubiria mrudiane na yeye? Kurudia matapishi ya EX ukitegemea amebadilika ni sawa na kupika sufuria la makande kwa mshumaa, utaambulia masizi tu. Kipi kipya kakiona kwako hadi arudi tena? Nini kilimshinda huko nyuma ambacho leo anakiweza anataka kurudi? Shtuka mtu wangu usije ukawa kipezeo au jamvi la wageni. KUWA NA MSIMAMO ukisema Its Over umaanishe, Sio unakuwa na hisia zinazopepea kama bendera ya katibu kata wa kishumundu. Mtu kama hakukuelewa tangu mwanzo achana nae, siku akijirudisha mwambie haupo kwaajiri ya majaribio ya kisayansj Usiendelee kutoa sifa mbaya kwenye napenzi etu "siku hizi hakuna mapenzi ya dhati" wakati wewe ndio hukuwa makini juu ya mapenzi yako. Huwezi kusoma degree ya law aalafu U-Apply kazi ya Chief Accountant wa bodi ya tumbak. Kila siku utasingizia balance sheet haina jurisprudence. Lawyersl Mmenielewa. Acha kudate watu wasiojielewa, Usidate kwa sababu uko Lonely, usiwe desperate kuingia mahusiano kwa sababu shosti zako wanakusimulia walivyopelekwa Kunduchi Beach. Ingia kwenye mahusiano pale moyo wako ukiwa tayari na mtu uliyemfia kihisia na amekuwa approved na veins, auricles, na aorta za oyo Wako kwamba He/She Is Really The One. Unadate na mtu ambaye mustakabali wake mwenyewe haujui, ukimuuliza anataka Kuwa aapi ndani ya miaka 5 Ijayo anakwambia Mungu anajua dont Worry, halafu BBM na Instagram unajiita Baby ake mie Iam in Love. Kuwa makini utaishia kutumika na kufua Boxer hadi.......... Date The Right Person,With Right Reasons, In A Right Time Uone Kama Mapenzi Hayapo Chukua hiyo then fanyia kazi.
 
MWANANGU HUTAKIWI KUOA MWANAMKE MPUMBAVU KAMA MIMI MAMA YAKO! Kijana mmoja alilelewa na Mama yake kwa shida sana, ingawa Baba yake alikua na uwezo mkubwa wa kifedha akifanya kazi nzuri lakini hakua akihudumia familia. Mama yake alifanya kila kitu yeye mwenyewe, alihudumia watoto, alisomesha na kufanya kila kitu na bado Baba alikua anakuja na kudai chakula. Baada ya kumaliza chuo kijana alipata kazi nzuri na kufanikiwa kuwa na pesa, siku moja alikua amekaa na Mama yake wakiongea. Mama yake alikua anamuambia aoe kwani anahitaji mjukuu na sasa ana maisha mazuri. Kijana alimjibu. “Mama natamani kuoa sana lakini wanawake wasiku hizi si wavumilivu, natamani kupata mwanamke ambaye atakua kama wewe Mama…” Kabla ya kumaliza kuongea kijana alishangaa Mama yake kumtandika kofi la nguvu usoni. Kijana alishtuka, hakujua sababu za kupigwa. Alinyamaza na hakuendelea kuongelea lile swali tena. Siku moja alishindwa kuvumilia, kile kitu kilimuwasha na kuamua kumuuliza Mama yake ni kwanini siku ile alimpiga kofi Mama alimjibu. “Hivi mwanangu shuleni ulienda kufanya nini? Pamoja na kusoma kote huko hujui ni kwanini ulisoma kwa shida? Mwanangu omba mke lakini usiombe mwanamke mpumbavu kama mimi Mama yako la sivyo wanao watateseka wakati wewe ukiharibu pesa huko kuhudumia watoto wa wenzako.” “Kivipi Mama, mbona wewe ni Mama bora na ulitulea kwa upendo?” Kijana aliza kwa wasiwasi akisogeza uso kukwepa kofi jingine. “Kweli Mimi ni Mama bora lakini si mke Bora. Nilimchekea Baba yako na kuruhusu akanipiga, nikamchekea wakati pesa zake akihudumia Malaya mimi nilimlisha na kumvisha. Akiishiwa nilikua namchukulia mikopo anaenda kuichezea na kurudi hana kitu, nilibeba majukumu yake na kumuacha yeye kwenda kubeba majukumu ya wengine. Mwanangu ningekua mke bora ningemlazimisha kuhudumia wanae. Ningeacha kumsaidia majukumu yake ili atambue wajibu wake. Lakini sikufanya hivyo nilimuendekeza kua atabadilika mpaka tukazeeka nikawa siwezi kuondoka tena. Hivyo mwangu huhitaji mwanamke kama mimi, unahitaji mwanamke ambaye atakukumbusha majukumu yako na kukufanya uwajibike kwa wanao. Ukipata mwanamke kama mimi utatelekeza familia yako na wanao watakuchukia kama ninyi mnavyomchukia babaenu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…