Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1.Itasaidia afya ya utumbo wako.

Unapojiona unaongezeka uzito ni kwa sababu machine yako haifanyi kazi vizuri, Imezidiwa na kiwango cha vyakula unavyokula, kwa nini? Kwa sababu hata bacteria waliopo ndani ambao husaidia uweze kupata choo, hawana afya ya kutosha kwa kuwa umewazidishia kazi yao. hawapati muda wa kupumzika
 
2.Inasawazisha Sukari ya damu

Ni ngumu na Sio rahisi kupunguza sukari inapokuwa imeingia ndani ya mwili wako, unapokuwa na presha, kuumwa mgongo, miguu, kiuno. Lakini kama ukiwa mtu wa kutumia muda vizuri hutaweza kukutana na magonjwa haya kwa sababu wewe utakuwa ni mtu wa kupigana na UJINGA sio mtu wa Kupigana na Umasikini.
 
Ukipigana na ujinga ,huwezi kukutana na magonjwa kama hayo hapo juu, hutaweza kuwa na uzito mkubwa, utautoa wapi ikiwa uko bize . Ugonjwa utaingiaje kwa mtu aliye bize kutafuta taarifa nzuri, anayekaa kufikiria na kuandika mawazo yake na kuchora ramani ya matarajio yake.Anafikiria atawasaidiaje wengine kupiga hatua hapo walipo. Ni wapi ugonjwa utamkuta mtu kama huyu? ni wapi ataweza kuwa na uzito mkubwa?
 
3.Itaondoa njaa Isio na sababu.

Siku hizi vyakula vipo kila mahali. Tena vinaonyeshwa kwa nje , vinavutia macho na kuongeza hamu ya kutaka kula. kwa maneno mengine, Ubongo wetu umeshambuliwa na ladha ya vitu vitamu kila mtaa unaopita, inarahisisha dalili za njaa kuanza kwenye akili zetu. Kwa hio watu wanashindwa kuelewa kama ni njaa au sio hali ya njaa bali ni tamaa ya macho na kushambuliwa kwa ubongo.
 
Usipopangilia masaa yako vizuri , hutaweza kupunguza uzito ulionao. Dawa kubwa ya kupunguza uzito wako ni kujua kutumia muda wako vizuri. Usiwe mtu wa kukaa muda mrefu bila ya kufanya kitu chochote. Anza leo kupunguza muda wa kukaa kijiweni kuongea habari za mpira, acha kukaa barazani kuongea umbea, acha kukaa kwenye Tv muda mrefu kutazama movies. Badala yake soma vitabu, nenda kwenye seminar mbalimbali, tafuta makala nzuri jifunze kupigana na ujinga. Acha kupigana na umaskini. Hutaweza kusikia njaa hovyo hovyo kama utafanya hivi vitu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…