Kwamba kila Dereva sasa atatakiwa kutembea na Leseni yake ya Udereva pamoja na Cheti cha Mafunzo ya Udereva...hii ni kusaidia kubaini na kukomesha Waliopata Leseni Mezani.
"Leseni Mezani".. tujiulize kwa Pamoja Meza hii inayozungumzwa hapa ni ya Nani?..Meza ya Raia, taasisi binafsi, Serikali au Vyombo vya Dola?
Kifupi Leseni ya Udereva inatolewa na Mamlaka iliyo Chini ya Serikali pekee ila Cheti cha Mafunzo ya Udereva kinatolewa na Vyuo vya Udereva ambavyo Asilimia 99.9 Vinamilikiwa na Watu Binafsi....Sasa kama Raia ana Access ya kupata Leseni ya Mezani kirahisi tu toka ktk Mamlaka na Vyombo vinavyosimamia Sheria, je Raia huyu atashindwaje kupata Cheti cha Mafunzo bila kusoma toka kwa Taasisi zisizosimamia Sheria kama vile Baadhi ya Vyuo vya udereva visivyo na uaminifu..?,...Watu Watapiga sana Hela.
Ukakiki hovyo kabisa kuwahi kutokea