Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Leo Ijumaa Julai 27, 2018, linatarajiwa tukio la kupatwa kwa mwezi.

Wakati wa tukio hilo, nuru ya mwezi mkamilifu (full moon) itazuiwa na Dunia hivyo mwezi kuonekana kuwa na rangi nyekundu kwa saa kadhaa kuanzia saa 4:30 usiku hadi saa 6:14 usiku.

Tukio la kupatwa kwa mwezi linatarajiwa kuonekana vizuri katika maeneo mengi ya bara la Afrika, Asia na Ulaya.

Hapa nchini Tanzania tukio hilo linatarajiwa kuonekana katika maeneo mengi na linatarajiwa kudumu kwa takribani saa mbili.

Kupatwa kwa Mwezi hutokea wakati Dunia, Mwezi na Jua vinapokuwa kwenye mstari mmoja.

Hali hiyo inapotokea mwanga wa jua unaofika katika uso wa mwezi huzuiwa na duara la Dunia.

Katika mpangilio huo nuru ya Mwezi huonekana kuwa na giza (Total Lunar Eclipse).

Hali hiyo inatarajiwa kujitokeza katika maeneo ya bara la Afrika, Asia na Ulaya usiku wa leo Ijumaa.
 
FB_IMG_1532669504275.jpg
 
Back
Top Bottom