Dawa hizo, Dynaval Co 80 / 12,5mg, Dynaval Co 160/ 12.5mg na Dynaval Co 160 /25mg; pia hutambulika kwa jina la soko la Valsartan Co, au Hydrochlrothiazide.
Dawa hizo zinazozalishwa China, zimeshapigwa marufuku na kuondolewa sokoni katika nchi za Afrika Kusini, Marekani, na Uingereza.
Taarifa ya TFDA iliyotolewa jana inaeleza kuwa imewataka wagonjwa wa shinikizo la damu kuacha kuzitumia dawa hizo na kwenda kwenye vituo vya afya ili wabadilishwe dawa.