Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mourinho pia alimpiga kijembe Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye misimu miwili iliyopita alimkejeli kutokana na uhamisho wa rekodi ya dunia kwa kiungo Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Old Trafford wakati aliponunuliwa kwa dau la Pauni 89 milioni.
 
Nina furaha kutabasamu na kuona hilo, unajua unaweza kubadili mtazamo wako, pia kubadilika kama mtu. Inachekesha lakini poa tu,” alisema kocha huyo Mreno ambaye anasifika kwa kuanzisha bifu mbalimbali na makocha wa timu pinzani. Hata hivyo, Mourinho alikiri Liverpool wamefanya uwekezaji mzuri katika kikosi chao na kudai wamenunua wachezaji wenye ubora mwingi ambao watawasaidia katika kikosi chao msimu ujao.
 
Nadhani kama una pesa inabidi uwekeze vizuri, ni bora kuliko kuziweka benki kwa sababu riba ni ndogo sana. Tatizo inabidi uwekeze vizuri na kwa kweli nadhani wamefanya vizuri kwa sababu kila mchezaji waliyemchukua ni bora na nina furaha kwa walichofanya,” alisema kocha huyo mtata.
 
Wababe hao wanatazamiwa kucheza pambano lao la kwanza la Ligi Kuu ya England Desemba 15 na Liverpool watakuwa wenyeji katika pambano hilo litakalopigwa katika dimba la Anfield wakati pambano la marudiano linatazamiwa kuchezwa Old Trafford Februari 23 mwakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…