Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

tapatalk_1532879210372.jpeg
 
Unafahamu hilo?

Lisha akili yako nguvu ya mawazo mazuri ili ufurahie maisha.

Wengi wetu hatujui hili, Na hata kama tunajua, Hatuamini katika hili, kwa sababu inaonekana haiwezekani. Lakini nataka nikuambie kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu kuamini. Hata kile unachokifikiria kinaathiri maisha yako pia.
 
Maisha yetu ni matokeo ya mawazo yetu.

Kuwa makini na mawazo yako, yanakuwa maneno;

Kuwa makini na maneno yako yanakuwa vitendo;

Kuwa makini na vitendo vyako vinakuwa ni tabia;

Kuwa makini na tabia , yanatengeneza Uhusika;

Kuwa makini na uhusika , yatakuwa ndio hatima yako.
 
Napenda kujaribu kujua baadhi ya mambo muhimu ambayo ukweli ni kwamba ni ngumu kuamini.Ni juu yako wewe kama unataka kuamini au hapana.Hasa kama unahitaji mabadiliko katika maisha yako unahitaji kuamini ukweli huu. Kama maisha yako yanakuwa mazuri kila siku, unaweza kuyafanya yawe mazuri zaidi, kwa sababu ni haki yako kuwa na maisha mazuri. Kama maisha yako yamekuwa hivyo zaidi ya miaka 5 bila ya maendeleo, basi unapoteza sana.
 
Anza kwenye fikra zako, na kila kitu kitakuwa sawa, kila kitu kitabadilika automatically. Kama utajifunza jinsi ya kulisha akili yako na mawazo mazuri. Epuka kulisha akili yako mawazo mabaya.

Unaweza usiweze kubadilisha hali ya ulimwengu kiuchumi au kisiasa.

Huenda usibadilishe hali ya hewa mahali unapoishi. Huenda usiweze…
 
Kuna mambo mengi ambayo hutaweza kuyabadilisha, hata kama utatumia pesa nyingi, hata kama una nguvu ya silaha kiasi gani.

Lakini kuna kitu ambacho unaweza kukibadilisha na kukifanya kiwe bora na bora zaidi kila siku. Na kubadilisha hiki , kitabadilisha maisha yako: Akili yako.
 
Wewe ndio mmiliki wa akili yako na mawazo yako, unaweza kuyathibiti.

Unaweza kuwa na fikra nzuri na akili nzuri kila wakati. Unaweza kufanya kinyume chake pia.kama akili yako imejaa mawazo mabaya yatakusumbua muda wote, lakini una uwezo wa kubadilisha ni rahisi sana.

Mawazo mabaya yamekuwepo ndani yako kwa muda mrefu, unayatumia, yanakuja, yanajenga kwa sababu umeyaruhusu kufanya hivyo.
 
Kwa nini usiwe na positive thoughts badala ya negative? Kuna faida gani unapata kutokana na hizo negatives?

Hasara unayopata kutokana na hizo ni kukosa furaha ya maisha. Yamechukua furaha yako.

Kuna zaidi ya kukosa furaha, yameleta huzuni, kushindwa. Kama unahisi kukosa bahati ni kwa ajili ya mawazo yaliopo ndani yako.Kwa hio badilisha mawazo na maisha yako yatabadilika na utaweza kupata kitu unachostahili.

Unastahili kuwa na maisha mazuri, haijalishi ukoje, una umri gani, unatoka wapi, na kitu gani umekuwa ukifanya .
 
Utafanyaje Hivyo?

Ni rahisi kuliko unavyofikiria. Unahitaji tu kuacha kufikiria mabaya na kusema mabaya yenye dalili yoyote ya ubaya, badala yake Akili yako na maongezi yako yajae mawazo mazuri na mema.

Usiongee kabisa kuhusu mabaya na matukio mabaya katika maisha. Kama ukifanya hivyo utakuwa unalisha akili yako mawazo mabaya, yatabakia akilini mwako, ni kama kuyamwagilia magugu ambayo huyataki yawepo bustanini mwako. Ni sawa na kukataa kuruhusu mawazo mabaya kuharibu akili yako.
 
My sister stop asking guys what they do for a living, they will lie,,, just take them to bed and count how many round they can go
1 round - rich guy
2 rounds - doing well in life
3rounds - unemployed
4rounds - broke as hell

THANK ME IF YOU WANT[emoji124][emoji124][emoji124]
Thank u[emoji23]
 
Back
Top Bottom